Social Icons

Wednesday 8 January 2014

ELIMU YA BURE: TAMBUA KUNDI LA DAMU ULILOPO , SOMA HAPA


Katika pekua yangu nimegundua leo hii kuwa watanzania wengi hatujui tupo
katika kundi gani la damu.

Na mbaya zaidi utakuwa wakina mama wana kundi labda -O, au kundi lenye
Negative huwa wanajifungua mtoto mmoja tu halafu hajifungui tena au
wakijifungua mtoto akifa hawajifungui tena, hii inatokana na kutojua kundi
la damu la mama na kundi la mtoto aliyezaliwa, kama mama hatapimwa na
kujulikana kundi lake la damu basi ataonekana tasa, hazai.

Kinachotakiwa kufanyika ni mama kutambua kundi lake la damu, na
atakapojifungua tu mtoto naye achukuliwe damu kwa ajili ya kujua kama
wanafanana kundi au laa. kama hawafanani ni lazima mama achomwe sindano
pale pale inayoitwa Ant-D ili imuwezeshe kupata ujauzito tena na
kujifungua. Bila hivyo mama kupata tena ujauzito ni hadithi na atatembea
sana kwa waganga, hospitali, makanisani akitaka msaada kama hawajagundua
hili.

Nawashauri watanzania wenzangu tupime ili tutambue makundi yetu ya damu.
Imeandaliwa na Buberwa Robert Blog

7 comments:

  1. Asante kwa sasa tumeelewa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nashukuru sana kwa uelewa wako, naomba endelea kuwa pamoja nami ili tupeane mawazo zaidi.

      Delete
  2. Mheshimiwa!! Na mimi ni B+ je inakuwaje kupata mtoto wa kiume na wa kike? ni mimi spika

    ReplyDelete
    Replies
    1. Spika mheshimwa wangu karibu ofisini, utapata majibu yako vizuri. Endelea kuwa nami katika kupeana mawazo

      Delete
  3. Hii elimu nzuri wengi tulikuwa hatujui haya

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nashukuru Mkama, ninakuahidi kukuletea elimu nyingine nyingi tu, tuwe pamoja ili tuendelee kupeana mawazo mazuri zaidi.

      Delete
  4. Hii elimu nzuri mkuu wengi wetu tulikuwa hatuyajui haya

    ReplyDelete

Asante kwa ku Comment yako ujumbe wako ni muhimu