Kwale (pia kware) ni ndege wa jenasi mbalimbali katika familia ya Phasianidae. Spishi nne za Francolinus ambazo zina ngozi kichele yenye rangi kali kooni na pande zote za macho huitwa kereng'ende pia. Rangi ya kwale ni kahawia au kijivu na wana michirizi au madoa. Mara nyingi miguu yao ni myekundu au rangi ya manjano na koo lao ni jekundu, jeupe, jeusi au rangi ya manjano. Hujificha kwa kawaida lakini sauti yao husikika mara kwa mara. Chakula chao ni mbegu, wadudu na nyungunyungu. Hutaga mayai matatu hadi kumi ardhini pengine juu ya manyasi makavu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Asante sana mkuu kwa kutuelimisha nimeipenda hii blog inafaa kusomwa hata na watoto sio kama zile nyingine
ReplyDelete