Kama tulivyoambizana kuwa blog hii itakuja na mambo yanayojulikana lakini
hayafanyiwi kazi kwa kuwa watu wamezoea tu kuishi basi leo natoa somo hili
ili kukukumbusha usifanye haya wakati umemaliza kula ili usijekupata
matatizo.
1. USILALE BAADA YA KULA
Usilale pindi tu mara baada ya kula, kwani chakula ulichokula hakitaweza
kusagwa vizuri na huweza kusababisha vidonda vya tumbo(Ulcers) na
magonjwa mengine ya kuambukiza kwenye utumbo mdogo.
2. USINYWE CHAI
iwe mchana au usiku, usinywe chai. Kwa mujibu wa utafiti, majani ya chai
yana kiwango kikubwa cha tindikali (Tannic acid), hivyo unapokunywa chai
tindikali hiyo hufanya protini iliyo kwenye chakula ulichokula kuwa ngumu
na hivyo kutosagika tumboni haraka, matokeo yake ni mtu kukosa choo kwa
siku kadhaa.
3. USIOGE
Usioge baada ya kula, oga kabla ya kula. Inaelezwa kuwa unapooga baada ya
kula, mtiririko wa damu huongezeka zaidi sehemu za mikono, miguu na mwili
na kusababisha damu kupungua sehemu za tumboni. Damu inapopungua tumboni
maana yake ni kudhoofika kwa mfumo wa usagaji chakula tumboni.
4. USILE MATUNDA Usile matunda baada ya mlo kwani ulaji huo hulifanya tumbo kujaa hewa na matokeo yake kusababisha gesi tumboni. Kula matunda saa moja au mbili kabla au baada ya kula chakula chako. Kula matunda muda mfupi tu mara baada ya kula chakula ni kosa ambalo linafanywa na watu wengi na huonekana ni sawa. Nakushauri ndugu yangu usiseme aah huyu naye, ANATANGAZA BIASHARA sasa nimekula halafu kazini natakiwa haraka, nenda kale matunda yako kazini jipe saa moja au mbili halafu ibia dakika 3 kula matunda yako. Mwisho utaambiwa kuna virutubisho shilingi laki(HAPA IWE LAKI TISA, SIO LAKINI) tisa utashangaa, wakati uharibifu wa mwili unaufanya mwenyewe.
5. USITEMBEE MARA BAADA YA KULA
Kutembea tembea mara baada ya kula husababisha mfumo wa usagaji chakula
kukosa uwezo wa kunyonya virutubisho vilivyomo kwenye chakula tunavyokula.
Badala yake tulia sehemu moja. Inashauriwa usitembee zaidi ya hatua 100.
6. USIFUNGUE MKANDA GHAFLA
Ni jambo la hatari sana kwa afya ya mtu. Mara baada ya kula, usifungue
ghafla mkanda wa suruali yako, uache kama ulivyokuwa hapo awali kwani kwa
kufanya hivyo kunaweza kusababisha utumbo kujikunja na kuziba.
7. USIVUTE SIGARA
Sigara ina madhara kiafya, tunashauriwa kuacha kutumia. Lakini inaelezwa
kuwa madhara yake huongezeka mara kumi iwapo mvutaji atavuta mara baada ya
kula chakula. Utafiti wa kimaabara unaonesha kuwa ukivuta sigara moja
baada ya kula ni sawa na mtu aliyevuta sigara 10, hivyo hatari ya kupata
saratani huongezeka kwa asilimia kubwa.
Ndugu yangu binaadamu tuna utashi, akili, maarifa.
Wanyama wamepewa
akili ndogo zaidi yetu, kwanini wanyama watuzidi, maarifa, akili hadi
utashi sasa. Somo hili linakukumbusha kuwa kwa muda mrefu unaishi bila
kufuata mfumo wa maisha unayotakiwa kuishi.
Tafadhali kuanzia sasa
unaposoma hapa badili mfumo wako katika ulaji, na nina kushauri kama una
tatizo lolote linalohusiana na tumbo mfano Kukosa Choo, Vidonda vya tumbo,
Gesi Tumboni, Miguu kuwaka moto, Homoni kuvurugika (wakina mama),
kisukari, nguvu za kiume, nguvu za kike, kuumwa sana kichwa, kitambi,
kulala usingizi bila kupenda, hii yote ni sababu ya mifumo mibovu ya
ulaji wa chakula, wasiliana nami kwa ushauri na kupata virutubisho
vitakavyokurekebisha na kurejea katika hali yako kama zamani.
Maoni yako ni muhimu.
Imeandaliwa na Buberwa Blog
No comments:
Post a Comment
Asante kwa ku Comment yako ujumbe wako ni muhimu