Social Icons

Friday 10 January 2014

MAWAZO HUZAA UKWELI; VIJANA MPO? SOMENI HII! KISHA JITAMBUE


Kijana mdogo wa sasa anawaza kula bata, sijui wana maana gani bata ukimuangalia ni mchafu mawazo yake ya ajabu ajabu fuatilia utaona.
 
Siku hizi fasheni kuwa shabiki wa chama au timu inayofanya vizuri kuliko kuyatafuta hayo mazuri ili tuwe na maendeleo.  Na unamkashifu kabisa mwenzako kisa timu yako imeshinda jana, au chama chaka unaona ndio kinajua kuliko kingine, hivi kwanini tusioneshane umwamba kwa kuwa hata na fire
extinguisher katika nyumba zetu za kupanga au tulizojenga? Kwanini usituite vijana wenzako tuje shambani kwako kununua mananasi yaliyokuzidi kwa wingi ili upate fedha na sie tupate mananasi, ni mtazamo tu lakini kuna mengine mengi
Katika maisha yangu hadi nimefikia umri huu nawaza kuwa na hotel ndogo tu hata isiwe na vyumba vingi lakini nashindwa  kwa kuwa sikuwa na mipango iliyo na umakini, miaka 40 nawaza tu niwe na hiki niwe na kile.  Lakini unakuta kijana mdogo wa miaka 26 tu akiwa anamiliki hotel  yenye akili ingawa si kubwa sana lakini unamuona kabisa kwamba ni mtu anayewaza na wazo lake limezaa.
 
Angalia hotel yenyewe ninayokuambia halafu utaniambia ninachozungumza.
 
Napenda sana kuona vijana tukiwa na maendeleo, tena maendeleo ya kutolea jasho la njia ya halali na si njia za panya kama wengi tunaoona na kusikia kuwa wamekamatwa, wamefungwa, wameharibika akili na miili.

Huu ni wakati wa mabadiliko ya fikra na si ku kaa chini na kuanza kulia kuwa wachina, sijui wawekezaji wan je wanachukua nafasi zetu, tupambane kuweza kujiingizia vipato kwa kuwekeza mawazo yetu, mitaji yetu, akili zetu, fedha zetu na uaminifu wetu katika shughuli za maendeleo ya kifamilia hadi kitaifa. Maendeleo hayaji kwa kuaihidiwa na baba, mama, kaka, mwanasiasa. Maendeleo yanakuja pale wewe unapozaliwa tu, umeletwa kwa kusudi maalumu na si kukaa kijiweni au barazani na kunyoosha miguu kama mikia yap aka huku unalalamika Fulani hafanyi hili, Fulani hafanyi lile. Tukimchagua Fulani ndio ataweza, aisee unajidanganya ndugu yangu. Ukitaka kuamini hilo wewe endelea kukaa na kulalamika na kuchagua viongozi wa kukupa maendeleo ndio utanielewa.
Napenda kumpongeza kijana huyu kwa kutumia mawazo yake, ndoto yake, ubunifu wake, na kufikia hapo kwa njia sahihi aliyotumia.  Napenda kumuambia kuwa “ Napenda maendeleo yako, ila utanisamehe natamani kukuzidi”
 
Nikipata ruhusa nitaongea naye na atatufundisha njia alizotumia kufikia hapo alipo, vijana ni wakati wetu huu sasa kubuni na kuiga mema yatakayotufanya tuwe matajiri kwa njia sahihi.  Nipo tayari muda wowote kuchangia mawazo ukiniomba katika mambo yenye tija na si kuniletea hadithina ulalamishi.  Nipo tayari kuwa na rafiki mmoja muelewa kuliko 100
wabovu, jifunze kutoka kwa walio endelea ili nawe uendelee.

Imeandaliwa na Buberwa Robert 

No comments:

Post a Comment

Asante kwa ku Comment yako ujumbe wako ni muhimu