Social Icons

Wednesday, 15 January 2014

SIRI HII HAPA: HAYA NDIYO MAFANIKIO AMBAYO HUYAFAHAMU NA UNAYAPATA KATIKA BIASHARA YAKO.


Wote tunapenda biashara zenye mafanikio, lakini hatujui tufanye nini. Wengi tunaanzisha biashara ya kuiga tu, ingawa sijasema kuiga ni dhambi,basi utakuta salon hapa, pale, kule, nyuma, mbele pembeni yam taro wengine hata mteja akija anashukuru Mungu ndio anaagiza na chips kabisa ili afukie mashimo ya njaa.  Mbaya zaidi huduma kwa wate sio nzuri kwa kuwa biashara yenyewe haina lengo lolote zaidi mtu anajua kusuka, hakuna maandishi (Business Plan), lengo la biashara kuwa baada ya muda Fulani nikuze biashara yangu kwa kuongeza jingo labda nk.
 
Wengi tuna nunua magari ili yawe Taxi lakini hii Taxi haina mafanikio hata kidogo kwa kuwa dereva analalamika gari limekuwa si gari na sasa ni jinni, maana linbugia mafuta balaa, ukija kwa madereva wenyewe sasa hawana mission wala vision, wao ni kubambika tu bei mteja anapanda taxi mwaka mzima wewe umeng’ang’ania bei kubwa hadi anakukimbia, lakini kama ukijipanga kwa lugha, bei nzuri, service ya gari, uaminifu utafanikiwa.
 
Wakati najiingiza katika biashara nilikuwa nafanya kwa moyo mmoja kwa kutaka kushirikiana na wenzangu hata ikiwezekana tuchange tuweze kufanya biashara moja ambayo itazalisha na kupata faida kubwa.  

Lakini kumbe wenzangu walikuwa na malengo yao, walifanikiwa kuchukua mitaji kutoka kwangu na nilibaki masikini mwisho niliamua kuhamia katika biashara nyingine ambayo nilihisi itanizalishia.  Nilijiunga lakini bahati mbaya nilisahau kuwa hiyo biashara nipo na wale wale walioniangusha, na nilianguka kweli kwa kuwa nilipoteza fedha, nilipoteza marafiki,
niligombana na mke wangu, nilikuwa na madeni ambayo hadi leo ninaendelea kulipa.
 
Siri kubwa ya kufanikiwa ni kujifunza elimu ya namna ya kutafuta na kuendesha aina ya ile biashara unayotaka kuifanya, lakini pia ni vyema kubuni mradi unaoweza kuendelea, sio ule ambao unaanzisha leo, kesho unakufa.

Jambo linguine la msingi ni kujenga tabia  ya kuweka akiba.
Lakini la tatu kali zaidi ambalo wengi wetu huwa ni gumu ni ushirikiano wa watu zaidi ya wawili, ambao mna nia moja katika jambo moja mfano salon.
 
Ikiwa salon inahitaji vifaa vya kisasa basi hakikisha wazo lenu liwe la vifaa vya kisasa, mfano hesabu zenu ziangukie kuwa na viti 100 vya wateja wanaofanyiwa usafi wa nywele, viti 100 ambavyo kuna wateja, wanafanyiwa steaming, viti 100, ambavyo kutakuwa na wateja wanaoshwa miguu, viti 100 vya make ups, madawa yaliyoidhinishwa na TBS na TFDA ambayo hayadhuru mteja, huu ni mfano tu na pia unawea kuona katika picha nilizoweka.

Mnapokuwa mmeungana nguvu inakuwa ni kubwa kazi yenu ni kusimamia kila mmoja kujua anafanya kazi kwa umakini, analipwa kama mkataba unavyosema, usafi wa ofisi, lugha nzuri kwa wateja, ratiba zinaenda kama zilivyopangwa, wahudumu wanakuwa na muda wa kupumzika na huku wakiwa huru

kwa wenye ofisi katika kusema yao yaliyo moyoni, mfano kutoa mawazo yao na yakanyiwa kazi, mikutano ya kila wiki mfano jumatatu na ijumaa huwa inazalisha utendaji kazi uliomakini, lakini mikutano ya kila siku asubuhi au jioni kwa wenye biashara ni muhimu.
 
Mnaweza kujiunga watu 10 mabao mtaamua kuchanga labda 5,000,000/= kila mmoja ukipiga hesabu 5,000,000 x 10 = 50,000,000/= mnaweza kupanga kimkataba kuwa tutafanya kazi kwa umoja kwa miaka mitano baada ya hapo tutaangalia kama inalipa ili tuendelee, au kila mmoja aende kivyake.
 
Ili upate mafanikio kwa karne hii ya 21, ni lazima uweke ushirikiano na wenzako bila hivyo utaimba kama nguchiro, na kila siku utabaki kukataa na kuona kila jambo ni baya katika biashara yako.
 
Kitu kingine kikubwa ni kuwa na muda au ratiba maalumu na inayotekelezeka katika biashara yako, mteja akija anataka baridi katika chumba iwe baridi sio kila siku wewe unakuwa mama samahani au baba samahani, hawa Tanesco hawa, hapana ingia mkataba na kampuni la umeme wa jua, au upepo, ili

wateja wako wapate huduma ile ile au zaidi ya ile na sio kila siku unapunguza ukarimu kisa anakuja kwako hana pa kwenda, weka vitu kama vinywaji hasa hasa sharubati za kutengeneza mwenyewe kwa matunda ya msimu na yale yanayopatikana iwe katika hali ya usafi.  Au chukua paketi moja ya Tanga Fresh mtindi na ndizi tano mbivu sana weka katika blender hakikisha una blend kwa sekunde 40 hadi 60, wape bilauri ndogo wateja wako wawili wanywe utaona kesho watakuja kuuliza kama ulinunua wapi kinywaji kile, maana utakuwa umewasaidia sana kiafya, na ladha pia.  Hili ni somo nitakupa baadaye.
 
Biashara sio kila dakika ufikirie kupiga hesabu watakuja wangapi wateja, biashara ni jinsi gani kwanza hawa ulionao wataendeleaje kuja ili nao wakuletee wateja wengi, weka motisha au zawadi kwa wateja akikuletea wateja 10 yeye atapata shampoo moja au shilingi 10,000 au hata kufanyiwa huduma bure.
Mafanikio hutokana na jitihada katika maisha tunayoishi. Watu wengi wanaopenda kufanikiwa hutafuta mbinu mbalimbali za kutimiza ndoto zao. Je wewe unafanya nini kutimiza ndoto ambazo umekuwa nazo kwa miaka mingi kwamba nataka kuwa mfanyabiashara mkubwa. 
 Waza unipe jibu, tupeane mawazo.

Imeandaliwa na Buberwa Robert 

No comments:

Post a Comment

Asante kwa ku Comment yako ujumbe wako ni muhimu