Social Icons

Monday 20 January 2014

JALI NYUMBA YAKO:JIFUNZE! MAJI KUJENGEWA MATANKI MAKUBWA KWA MATUMIZI MENGINE


Ndugu mwana Blog wa Buberwa Robert kama ilivyo ada, tunajaribu kupeanaamawazo kuhusu maendeleo katika nchi yetu.
Katika fikira zangu za njozi, njozi ya maendeleo, nina ota kupatawataalamu (Engineers) ambao watabuni jinsi ya kuyafuga maji kutoka popote pale na kuyapeleka katika visima vikubwa sana ambavyo vinaweza kujengwa















kwa matumizi ya maji kwa wananchi, kwa wenzetu wa Zimamoto (Hydrants), kwa matumizi mengine mengi ambayo wadau tutajadili.
Wazo langu linakujaje kuna mitaro mingi sana inachimbwa katika mabarabara na mitaani, lakini mwisho wa siku ile mifereji na mitaro inaangukia sehemu ambazo kiukweli hazina faida zaidi ya kutengeneza mafuriko makubwa yatakayokuja kuumiza wanadamu, kwa kuwasoma, kujaa katika nyumba zao, kuvunja majumba, kuleta magonjwa. Pia kuleta ugomvi kati ya wananchi na serikali kwa kuwa mwisho wa siku wataambiwa wahame, mara wasogee.
Naomba kama kuna uwezekano mainjinia wakune vichwa vyao na waangalie ni jinsi gani maji ya mvua yote yana vunwa na kupelekwa katika visima vikubwa katika wilaya zote, na vitongoji ambavyo vitateuliwa kuwa ajili ya matumizi ya maji hayo badala ya kuyaacha haya maji yatiririke tu aidha kwenda kwenye miti, mifereji mikubwa au yapotelee tu katika mabonde, simaanishi mimi najua sana ila naomba tupeana mawazo kuwa haya maji yavunwe kitaalamu.













Kuna sehemu maji ni ya shida sana wangeweza kutumia maji haya yakiwa yametengenezwa kitaalamu Leo nawaachia homework hii tujadili kwa ufanisi.

Imeandaliwa na Buberwa Robert Blog
 

No comments:

Post a Comment

Asante kwa ku Comment yako ujumbe wako ni muhimu