Mto Msimbazi ni mto mkubwa
sana ambao unaweza kutumika kwa usafiri, moja ya kupunguza adha ya foleni
barabarani ni kuutumia mto msimbazi kwa usafiri.
kuanzia
Salender Bridge, Muhimbili, Jangwani hadi Vingunguti, na sehemu nyingine
ulipopita. Wale watengenezaji plan za
miji wangeweza kufikiria jinsi ya kuufanya mto huu kuwa kivutia hapa Mkoani Dar
es Salaam, kwa kushirikiana na wataalamu wengine.
Kila ninapo
kaa na kuuangalia mto huu naona kuna kiasi kikubwa sana cha fedha mkoa kama
mkoa na wananchi wake tunakosa, pia ni sehemu nzuri sana kwa kufanyia sehemu za
burudani na mandhari nzuri zitakazo weza kuwavutia wawekezaji wa ndani zaidi na
nje kuweza kufanya biashara katika maeneo yaliyopita kwa kuweka Hoteli,
Migahawa, Nyumba za Kulala wageni, Sehemu za sherehe, Boti za kusafirishia
abiria, mandhari nzuri za bustani.
Mimi sio
mbunifu wa kuchora, wa kupamba lakini najua wapo wataalamu wanaoweza kutengeza
ramani, picha, na jinsi ya kuyatengeneza maji yaweze kuwepo muda wote kwa
kiwango kinachotakiwa ili boti ziweze kupita kwa miaka yote bila kuathirika na
upungufu wa maji au takataka. Nikiwa
kama mtanzania ninayependa maendeleo ninaiona Tanzania tofauti kidogo na
wenzangu kuna vitu vingi tunaweza kuvifanya katika mto huu wa Msimbazi na
tukaweza kupata kipato kwa uvuvi, usafiri na mambo mengine mengi yatayobuniwa
na kuwekwa pale, pia ni ajira kwa vijana, hapa ndipo pa kupatia ajira vijana
wengi.
Nadhani wazo
hili litakuwa na mantiki zaidi kama wataalamu wa Wizara husika na wananchi
watatumia busara, hekima na utashi walio nao na kugombea mambo yasiyo na tija,
tunaweza kwa silimia mia kuutumia mto huu kwa tija, na tusifikirie bonde la mto
msimbazi tu kama bonde, tufikirie mto kama mto, maana sasa hivi mto ule
hauonekani kwa kuwa umefunikwa na ujenzi wa vijijumba, majumba na kilimo, pia
na kuwa sehemu kubwa ya utupaji taka.
Sidhani kama kazi hizi ndizo zinazotakiwa kufanyika katika mto huu.
Kuna wateja
wengi sana ambao wanaweza kuutumia mto huu kuanzia mjini hadi vingunguti, kuna
mabilioni ya shilingi tunaweza kuyapata kupitia mto huu, ni kiasi cha kubuni
cha kufanya tu chenye tija. Nimetoa mada
moja inayosema jinsi ya kuyafuga maji tunaweza kuyafuga kwa kuyaingiza maji ya
mvua katika mto huu kwa faida na kuweza kuutumia na kuingiza kipato kwa mkoa
mzima.
Mkuu wa Mkoa,
Wakuu wa Wilaya, Wabunge, Madiwani, Mameya na Waziri wa Wizara zinazohusika
mnaweza kukaa na wataalamu mkapanga la kufanya ili itokee mwisho wa siku kuwe
na njia ya usafishaji wa kupitia mto Msimbazi, na msiwaze tu labda kuwe na uwazi
wa kutengeneza sehemu ya michezo, tuutumie mto huu kwa tija. Tusilifanye jambo hili kisiasa, tusiogope
wananchi kulalamika kwa sasa, ila mwisho wa siku wataelewa namaanisha
nini. Watanzania tunatakiwa kuwa
wabunifu na kuufanyia kazi ubunifu huu kwa manufaa ya nchi na wananchi na
mwisho wa siku tufaidi wote.
Wana blog wa Buberwa Robert Blog! tutoe mawazo kwa michoro na picha ili tuijenge nchi yetu.
Inawezekana kabisa Mto huu ukiboreshwa ukawa na faida kama baadhi ya mito hii hapa.
Wana blog wa Buberwa Robert Blog! tutoe mawazo kwa michoro na picha ili tuijenge nchi yetu.
Inawezekana kabisa Mto huu ukiboreshwa ukawa na faida kama baadhi ya mito hii hapa.
Ni wachache wanaweza kufikiria kwa kiwango hichi.
ReplyDeleteYes ni kweli, ila tukiungana tunaweza
Delete