BIASHARA
YA MTANDAO:
Biashara ya mtandao ni
biashara inayozaa na kuzalisha, ni biashara ya kuambiwa, kukubali, kutumia, na
kuwaambia wengine, ili nao wafanye kama ulivyofanya wewe yaani uwaambie,
wakubali, watumie nao wawaambie wengine. (DUPLICATION)
Leo nazungumzia
biashara ya mtandao kwa kuwa watanzania wengi kama bado hawajaielewa hivi na
walioielewa kama wanapotosha hivi baadhi yao.
Utakuta unatoa darasa
au unamuelezea mtu kuhusu biashara ya mtandao anakuja si ile kama kampuni
Fulani, huo ni unafiki sio kujua huko, kama uliskia kaa kimya mbona hukuanza
wewe. Msikilize anayetoa mada tena
katika wakati na sehemu inayoeleweka, kwanini naongea haya, kwa kuwa utakuta
wengi wa watu hawa kabla hujaendelea anaanza kuelezea kampuni ingine na kuanza
kuiponda au kuisifia, ingawa wengi utasikia ya nchi gani hiyo, hamna lolote
mimi nimeshatumia sana.
Biashara
ya mtando ilianzishwamiaka ya 1960s huko Marekani na mamilionea wengi wa
marekani walianza kushika milioni yao ya kwanza kwa kupitia Biashara hii ya
mtandao.
Kwa hapa kwetu Tanzania makampuni yanazidi kuja mengi na biashara hiyo inazidi kushika kasi kwa nguvu kutokana na wengi wanavyoonja mafanikio.
ukisikiliza watu wanavyoifanya biashara hii utakata tamaa na kuitwa machinga lakini kiuhakika na ukweli biashara hii haipaswi ubebe bidhaa uzunguke nazo kama machinga. Wengi tumeshindwa kuelewa biashara hii na ndio maana mtu akifanya baada ya miezi mitatu au minne anahisi haoni mafanikio mwisho anaamua kuacha na kusema biashara hailipi, wakati anafanya biashara hii kimakosa
Jinsi ya kufanya hii biashara ni kama nilivyosema ambiwa, kubali, tumia, muambie na mwingine, akubali, atumie naye amuambie na mwingine.
Ili
ufanikiwe katika biashara hii ni lazima kwanza uijue kampuni, mwenye kampuni,
bidhaa zake, na mfumo wa biashara yenyewe.
Biashara hii ni ngumu sana lakini wagumu ndio watakao baki. Tuna ushahidi wa wafanyabiashara wengi wa
biashara hii ya mtandao ambao wanapata kipato kikubwa mwisho wa mwezi, na
mwisho wa mwaka, wapo wanaopata hadi shilingi milioni 10 kwa mwezi, na mwisho
wa mwaka wanapata zaidi ya shilingi milioni mia mbili na zaidi (TSHS.
10,000,000 hadi 200,000,000) kama ulikuwa hujui jua kuanzia leo. Biashara hii ukiisikiliza unaweza kwenda
kukopa mabilioni ya shilingi ili uje upate yale yote unayoambiwa katika kampuni
ile, ni kweli wayasemayo yanapatikana hakuna mjadala, hakuna tapeli hata
kampuni moja katika zilizopo Tanzania, tatizo ni wafanyabiashara wameelewa
muundo wa biashara hiyo?
Wanajua jinsi ya kuwatafuta wateja? Je kuna idadi gani
ya watanzania walio na afya njema, kuna idadi gani ya watanzania wanaoumwa, na
je kuna idadi gani ya watanzania wanaoumwa huku hawatambui kama wanaumwa.
Angalia
taarifa hii ilitoka mwaka jana katikati yaani 2013, inasema hivi katika watu
bilioni saba (7,000,000,000) dunia 5% wana afya njema nao wana umri wa miaka
kuanzia 0 hadi 5 je wewe unayesoma umo humu kwenye hili kundi?. 20% ni wagonjwa waliolazwa Muhimbili, na Hospitali nyingine unazozijua ndani na nje ya
nchi pia na wale wanaotumia dawa kwa kutambulika. Na 75% ni wagonjwa watarajiwa au wanaotembea
na ugonjwa pasi na kujua na ndio maana utakuta wengi wetu tuna kufa ghafla
maana tuna magonjwa huku tunatembea na huku akili zetu nafsi zetu
zikitundanganya kuwa ni wazima wa afya.
Nikuulize swali! Lini ulisikia kitu kama radi kimepiga upande wa kushoto
ukashtuka ukakimbilia hospitali? Na lini
gari yako imelia kitu mvunguni tiii au umesikia mvumo huuelewi ukakimbia kwa
fundi? Acha unafiki jibu ukweli.
Huo
ukweli wako ndio utakuponya.
Kama
nilivyosema biashara hii ilianza miaka ya 60, sisi ndio inaingia sasa Tanzania
ndio maana tunashtuka hatuzijui vizuri kampuni hizi wala biashara hii, na
bahati mbaya biashara hii ya mtandao imekuja Tanzania na makampuni ya
virutubisho mengi au yote kuliko ya vifaa kama sufuria, umeme na
kadhalika. Wenzetu walio endelea
hukimbilia sana biashara hii kwa kuwa inalipa vizuri sana, huku kwetu hasa
Tanzania tunaikimbia kwa kuwa ni ya kujituma.
Biashara
ya mtandao inajenga asikuambie mtu, unajua mambo mengi kuliko unavyodhani, wala
usitangulize dharau kuwa hawa ni wamachinga sijui wanaongea sana hapana, tena
biashara ya mtandao hutakiwi kuwa muongeaji sana, unatakiwa kuwa mtumiaji sana
wa bidhaa ili wengine waone mabadiliko yako nao watamani kutumia bidhaa
unazotumia, ili nao wawe kama wewe.
KOSA KUBWA TUNALOFANYA WAFANYABIASHARA WA MTANDAO
Unaposikia
au unapoitwa katika kampuni ngeni au wewe ni mgeni katika kampuni ile basi kuna
wale wenyeji wanaokujua na kukuita pale basi hukuita kichwa, jembe kwa kuwa
wanaamini ukiingia utawabuzuta watu wajiunge na ile kampuni kwa kuwadanganya
mambo yasiyo ya kweli na kweli ili waingie na mwisho wakiingia hawaoni ulicho
maanisha kwa kuwa hayo uliyosema si ya kuonekana leo ni hadi miaka mitatu hadi
mitano, na kosa lingine ni kitendo cha kuanza kupiga hesabu kichwani eheeee
nimeambiwa kuna dawa ya kisukari nina shangazi ana kisukari, mjomba ana
kisukari, jirani ana kisukari, fulani ana matatizo ya hedhi, mama fulani ni
mnene sana, mama ndimu, ana vidonda vya tumbo, bi mkora ana pressure,
shekiangio ana tatizo la ngozi baaasi watakoma naenda kila mmoja anipe shilingi
laki nne nimpe full dozi, sasa utakuta mwana mtandao anaenda kwa wateja wenye
hela ili apate bonus, na points za mwezi bila kuangalia biashara hii haitaki
wagonjwa kwa asilimia kubwa, biashara hii inataka mtu atumie virutubisho hivi
kwa kuwa vyakula tunavyokula, maji na juice na pombe tunazokunywa zina sumu,
pia dawa karibu 90% zina kemikali hivyo tunatakiwa kutumia hivi virutubisho ili
kuondoa kemikali hizo.
Sasa hivi
kila chakula kila tunda, kila mboga inawekwa dawa, au mbolea zina dawa, hivyo
ni vyema kujifunza vyema bidhaa hizo ili kuweza kutafuta wateja wa kujiunga na
kuzitumia kwa mafanikio, tatizo sio kampuni na wala tatizo si nchi tatizo ni
sisi wasambazaji, tukitulia na kujifunza vizuri tutaisaidia sana jamii.
Hospitalini
ni sehemu ya kikinga maradhi, lakini sasa hivi ni kinyume, hospitalini ni
sehemu ya kutibu magonjwa tena yaliyoshindikana, elimu hizi ambazo zinatolewa
na makampuni ya virutubisho ilitakiwa itolewe na manesi na madaktari ili watu
wasifikie hatua ya kuumwa, figo, kuto kupata choo, moyo, macho, ngozi,
kutokupata hedhi, ulaji bora wa chakula bora, unywaji wa maji, unywaji wa
sharubati, utumiaji wa mboga za majani na kadhalika. Haya yote yanatakiwa
kufanywa na hospitali, lakini pongezi kwa wafanyabiashara wa biashara ya
mtandao wanafanya kazi kubwa sana kuelimisha jamii, ingawa jamii yenyewe nayo
kuelewa ni kazi sana, lakini naamini wataelewa tu.
BIASHARA
YA MTANDAO INAIINGIZIA SANA SERIKALI MAPATO
Kama
ulikuwa hujui basi biashara ya mtandao inaiingizia sana serikali mapato, maana
kampuni inapoingia nchini inafuata taratibu zote za kisheria, za ulipaji kodi
na inapewa TIN namba na inaingia katika usajili wa ulipaji wa kodi
kisheria. Ukitaka kujua hili zaidi
nitafute nikupeleke ukaone.
WAFANYABIASHARA YA MTANDAO WANAKOPESHEKA
Unapojiunga
katika kampuni yoyote ya biashara ya mtandao unajisajili na kuweka vielelezo
vyako vyote katika fomu, na pia kampuni inakutambua kuanzia katika nchi yako
hadi dunia nzima ambapo kampuni hiyo ipo, kwa kuwa unapofikia cheo fulani basi
kuna kamisheni unapata kutokana na cheo chako na wale wenzako mlio katika cheo
kile katika dunia nzima, hivyo gawio la pato la mwezi huo linagawiwa kwa ninyi
mameneja wote duniani. Vile vile
unapopanda cheo kimoja kwenda cheo kingine kampuni itakutambua na kukupa cheo
chako na dunia nzima itakutambua kwa kufikia hatua hiyo. Sasa nauliza mabenki yaliyopo hapa Tanzania
kuna siku mlishawaza kuwafuata wafanyabiashara wa mtandao na kupata darasa
kuhusu biashara hii inayoingiza mamilioni ya shilingi hapa nchini kila siku? Je
ikiwa sisi wafanya biashara wa mtandao tunatambulika nje ya Tanzania kwa nini
benki iliyopo Tanzania isinitambue? Naomba sana watu wa benki kama mnataka
faida kubwa nioneni mimi niwaoneshe wapi mnalosa wateja wengi wenye pesa nyingi
na wanaokopesheka na wenye uwezo wa kulipa halafu ninyi hamuwafuatilii. Biashara yoyote ambayo mfanyabiashara anaweza
kupata kuanzia shilingi 100,000 nadhani anakopoesheka bila matatizo kikubwa ni
kufuata taratibu, kanuni na sheria za mikopo.
Naamini
ikiwa benki zitatutambua na kutuamini tunaweza kukopa na kufanya biashara zetu
na kurejesha mikopo kwa wakati, kikubwa kinachotakiwa ni kupeana elimu tu.
Imani
yangu wanamtandao tukijiunga vikundi vya watu kuanzia 30 kama vicoba tunaweza
kupata mikopo mikubwa na kufanya mambo makubwa sana katika biashara hii.
Nakuomba
mdau unayesoma hapa kama utakuwa hujaelewa na una swali usisite kunipigia simu,
kutuma sms, au email ambazo zinaonekana katika mawasiliano hapo ili tupeane
mawazo zaidi.
No comments:
Post a Comment
Asante kwa ku Comment yako ujumbe wako ni muhimu