UFUGAJI WA KUKU
Mdau
wa blog ya hii.
Wengi
wetu tunafuga kuku pasi na malengo, nimekaa chini na nikaona uchoyo ni jambo
moja baya sana linalotuumiza sana watanzania katika maendeleo ya kila jambo.
(Hasa uchoyo wa mawazo, tunalaumu mno hatutoi mawazo yenye tija)
Leo
naongelea kuhusu ufugaji wa kuku, hasa kuku wa kienyeji ufugaji wenye tija.
Kuku
hawa ni rahisi sana kuwafuga lakini ni wagumu sana kama hutokuwa makini na kama
huna malengo na ufugaji wako. Wengi wetu
tunafuga tu huku tukiwa na matarajio makubwa ya mafanikio. Unajidanganya ndugu yangu, huwezi kutegemea
kitu ambacho hukipendi na hukigharamii.
Kuku wanatakiwa kula, kuku wanatakiwa kunywa, kuku wanatakiwa kupata
huduma za dawa, kuku wanataka kulala sehemu nzuri na safi, yenye hewa,
wanapopendwa, wanapojaliwa, kuku wanahisia kama viumbe wengine huwa wanapenda
wakiwa na shida uwaangalie kama unavyoangalia kitu kingine chenye uhai na
uwasaidie, lakini ukiwa mkaidi kwao nao watakuletea ukaidi. Haya ni maneno huwa naambiwa na mama yangu
mzazi bi Paulina, huwa anawaangalia kuku wangu na anasema hawa kuku wana shida
lakini huwaelewi, sasa nimeanza kumuelewa na ndio maana nataka nikupe elimu hii
nawe uweze kufaidika.
ONDOA UCHOYO KWANZA
Kama umeamua kufuga
kweli basi fanya haya, usiwe bahili wa muda kwa kuku wako, usiwe bahili wa vitu
vifuatavyo;
a.
Fedha za
kununulia chakula
b.
Fedha za dawa na
daktari
c.
Fedha kwaajili
ya kununua mboga za majani au ufanye kilimo cha mboga za majani ili uwalishe
d.
Fedha kwaajili
ya ulinzi wa kuku wako
e.
Fedha kwa
mtunzaji wa kuku wako
f.
Fedha za
usafirishaji kwenda kwa wateja wako, au katika manunuzi ya kuku wageni
Lakini
kuna jambo kubwa zaidi, umoja kati yako wewe na wafugaji wenzako.
Na
hii leo ndio mada yangu kuu.
Umoja
wa wafugaji katika eneo hilo ulilopo, ndio nguzo kuu ya kupata kipato kikubwa
zaidi na kuwa na soko kubwa zaidi mwaka mzima na miaka yote na hakuna mtu
anatakayekosa huduma ya kuuziwa kuku au mayai katika eneo lenu ikiwa mtakuwa
wamoja kwa ufugaji wa kuku.
LENGO MOJA NA MOYO MMOJA
Ni
vigumu sana kwa watu zaidi ya 100 kuwa na lengo moja kwa miaka zaidi ya 10,
lakini kama mtaamua na mkaona faida yake inawezekana tena kwa 100%. Naongea haya kwa kuwa naona kabisa ili
ufanikiwe kuwa kama unataka kuku 10,000 kwa kipindi kifupi ni ngumu lakini
wafugaji 30 mkiunda kikundi na mkachangishana labda shilingi 500,000 kwa kila
mmoja mtapata shilingi za kitanzania 15,000,000. Mkiamua sasa mjenge banda la shilingi
3,000,000 zitabaki 12,000,000. Na mkinunua chakula cha shilingi 3,000,000
zitabaki milioni 9,000,000. Wengi wa
wauzaji wa kuku huuza kuku waliochanjwa hivyo unaweza kukaa na kuku wale kwa
miezi mitatu zaidi wakiwa wako vizuri bila kuugua. Nunueni kuku kwa shilingi
1,600, leo nakupa siri kama ulikuwa hujui nipigie simu nitakuambia vizuri wapi
pa kununulia na utashangaa utakuja kuwa na kuku hadi ulie. Katika milioni
9,000,000 zilizobaki nunua kuku wa shilingi 5,000,000 kwa kila mmoja kumnunua
kwa shilingi 1,600 utapata kuku wangapi?
Utapata
kuku 3,125. Kuku hawa utawanunua wakiwa
na umri wa miezi mitatu na nusu, hivyo utawakuza kwa miezi miwili na nusu
wataanza kutaga. Lakini kama mtataka
kuwa na kuku wengi zaidi kwa muda wa miezi 6 mnaweza kuwa kundi lenu la watu 30
mkawa mnachangishana 200,000 kila mmoja ina maana kila mwezi mtapata shilingi
6,000,000 x 6 = 36,000,000.
36,000,000/1,600
= 22,500
Kundi
litapata kuku 22,500 ina maana kama kuku mmoja baada ya miezi minne atauza kwa
shilingi 10,000 kwa kuku 22,500 kikundi kitapata shilingi 225,000,000.
Kwa
maana hii kikundi kitakuwa kimepata faida ya shilingi;
225,000,000
– 36,000,000 = 224,964,000
224,964,000
– 50,000,000 = 174,964,000
Hiyo
hesabu ni makadirio na matumizi ya kilichopatikana ilitumika 36,000,000 kununua
kuku 22,500 wakauzwa kwa shilingi 10,000 kwa kila mmoja ikapatikana shilingi
225,000,000 tunatoa fedha ya manunuzi iliyokuwa shilingi 36,000,000 hivyo
itabaki shilingi 224,964,000 katika pato hilo la 224,964,000 toa 50,000,000 ya
vyakula, maji, mlinzi, mhudumu, umeme na maji utabaki na shilingi 174,964,000 (weka
hasara ya kuku wengine kufa) faida itakuwa 100,000,000
Hii inaweza kufanya
kila mwanachama wa kikundi akawa na faida ya shilingi 3,333,333.30 ambapo
mkiamua kujiwekea malengo ya kuuza kuku kwa mizunguko 1,000 kila mwanakikundi
atakuwa na faida ya shilingi 333,333,300 na hii inawezekana sana kama kundi
lina nia na linaupeo na si kulalamika kila wakati. Tatizo letu watanzania ni walalamishi sana
sio wote ila asilimia kubwa ni walalamishi.
Nina hakika kundi hili linaweza kujikwamua kwa kuku tu bila
kujichanganya na jambo lingine. Kundi
likijipa miaka mitano ya kufanya biashara hii kwa nguvu na nia itakuwa mfano wa
kuigwa.
Kumbuka kuna kundi la
kwanza la kuku 3,125 ambapo kuna shilingi 4,000,000 ilibaki benki kama kilinda
benki, kikundi hiki kwa mahesabu yale yale kina uwezo wa kutengeneza
shilingi na shilingi za mamilioni. Ila sasa huku itazitengeneza kwa kuzalisha
mayai ya kuku wa kienyeji.
MAYAI YA KIENYEJI
Ikiwa
kuku 3,125 majogoo yatakuwa 1,125 na
majike 2,000 basi una uhakika wa kuwa na trei 66 kwa siku. Chukulia mfano siku 7 za wiki unachukua mayai
manne tu kwa wiki utapata mayai 16 kwa kuku hii inamaana utapata mayai 32,000
kwa mwezi ambayo ni trei 1,066. Trei
moja ya mayai ikiuzwa shilingi 12,000.
1,066
x 12,000 = 12,792,000 kwa mwezi
12,792,000
x 12 = 153,504,000 kwa mwaka
Kwa
maana hiyo mayai yanaweza kuingiza shilingi 153,504,000 ukitoa gharama za
usafirishaji na mhudumu mnaweza ingiza 100,000,000 kwa kuuza mayai ya kienyeji
pekee.
Kwanini
tusijiunge tukafanya shughuli hii?
Unasubiri
nini?
Unataka
kuona nimetajirika kwanza ndio na wewe uhamasike?
Usiwe
mchoyo njoo tujiunge tukuze kipato kwa biashara hii niliyokupa sasa hivi
MBOLE YA KUKU
Kinyesi cha kuku ni mbolea nzuri sana kwa wakulima,
kwa idadi ya kuku iliyopo katika kikundi na inayoendelea kuwepo kila mfuko wa
mbolea ya kuku inauzwa shilingi 2,000.
Ikiwa kikundi kitakuwa na mifuko isiyopungua 2,000 basi kikundi
hakitakosa shilingi 4,000,000 iliyotokana na mbolea.
Mifumo mingine utaweza kuipata tukiwa wote katika
kikundi na tutaibuni zaidi na zaidi. Kwa
leo niishie hapa, nashukuru kwa kusoma wazo langu, ninaomba mawazo yako na
tuyafanyie kazi ili tujikwamue kiuchumi.
Mawasiliano yangu yanapatikana katika blog yangu
moja kwa moja karibu, ila bahati mbaya simu yangu namba +255765903379 imepata
shida kidogo sitakuwepo hewani kwa muda, iwe katika WhatsApp, Instagram naomba
radhi kwa usumbufu ila namba nyingine zote nipo hewani
No comments:
Post a Comment
Asante kwa ku Comment yako ujumbe wako ni muhimu