Habari
ndugu msomaji wa blog hii.
Uvuvi
katika nchi yetu hii ya Tanzania unachukuliwa kama utani, unachukuliwa kama mtu
akishindwa maisha basi anaingia majini na kwenda kuchukua samaki na kuleta nchi
kavu ili wateja tununue.
Uvuvi
wa samaki ni kazi tena kazi yenye kipato kikubwa sana katika dunia hii. Wengi wa wavuvi wetu wanawaza kuchukua
mitumbwi na kuanza kupiga makasia kwenda baharini kuvua samaki, lakini sidhani
kama kuna wanaokaa na kufikiria kununua meli kubwa zenye uwezo wa kubeba tani mia mbili na
hamsini na kuendelea za samaki kwa siku.
Samaki wenye minofu na wanaotakiwa katika soko ni ni wale walio katika
kina kirefu na umbali mrefu ambao boti zetu hizi tunazotumia haziwezi kufika,
na hata zikifika huko basi hawawezi kumudu nguvu za maji hayo.
Uvuvi
wa kusafiri umbali mrefu na meli kubwa zenye uwezo mkubwa ni njia pekee ya
kumnyanyua mvuvi katika uvuvi wake wa samaki, kuna samaki wengi wanaotakiwa
katika soko. Soko ninalo zungumzia hapa
ni la ndani na la nje ya nchi.
Ikiwa
meli itakuwa na uwezo wa kubeba tani 200 basi kuna uwezekano wa kutengeneza
kiasi kikubwa cha fedha kila siku katika uvuvi.
Ikiwa wale samaki walioitwa wa Magufuli walikuwa tani 296.32 wenye
thamani ya shilingi bilioni 2.07. ina maana wale samaki walikuwa kila kilo ni
shilingi 7,000.
7,000
kwa kilo. Chukua meli ina tani 296.32,
tani moja ni kilo 1,000 x 296,320 = bilioni 2.07 je wale samaki tunaovua pale
ferry, na msasani wanafika bei hii kwa siku au wiki? Kama ndio basi wavuvi
wamelogwa, kwanini hawaendelei?
Mada
hii naiandika nikiwa nawaza kwa uwezo wangu, je kwanini mdau wewe usiidadavue
biashara hii ukaona kama inalipa tujiunde kama kikundi kikubwa tununue hata
meli moja kubwa (30.2m longline fishing vessel) ambayo ni kama shilingi za
kitanzania milioni 500 meli inaweza kuingiza bilioni 2 kwa wiki, hatuoni kuwa
tunapoteza muda sana?
Ikiwa
wadau 100 tutachanga shilingi 5,000,000 tutapata kiasi cha shilingi 500,000,000
ambacho tunaweza kuagiza meli hii na kufanya taratibu nyingize za kisheria na
tukaanza rasmi kazi ambapo meli hii hata kama itaingiza shilingi bilioni 2 kwa
mwezi ina maana kwa miezi 12 tutakuwa na shilingi bilioni 24 sasa hapo mdau
utakataa kuwa mmoja wa wawekezaji wa meli hii, na hapo tunaweza nunua meli 4
zaidi ambazo zitakuwa zinafanya kazi kwa masoko yote ya samaki. Samaki watakuwa wakubwa wenye bei rahisi na
si visamaki vidogo vya bei ghali tena samaki watazaliana sana kwa kuwa wale
wakubwa ndio watakao fuatwa. Tunaona
wavuvi wengi sana wanavamia sehemu za mazalia ya samaki hii inachangia hata
kupotea kwa samaki hata katika misimu yao.
Huwezi kupiga vita kuvua samaki kwa net ikiwa wavuvi wana waza leo,
kesho Mungu atajua, ni lazima tuwe na mawazo mapana ili tuweze kutokea upande
wa pili wa mafanikio.
Serikali
inakosa mapato makubwa, wavuvi wanakosa kipato kikubwa, wateja wanakosa samaki
wenye ladha na ubora kwa kuwa hakuna vitendea kazi, manahodha wapo wengi meli
chache, ikiwa kundi litanunua meli 4 kuna ajira 4 za manahodha, na mabaharia,
wavuvi kwa nafasi zao, hapa tutakuwa tumetengeneza ajira pia. Tutakuwa tumeongeza kipato kwa nchi, kipato
kwa familia na kadhalika.
Mdau
hebu kaa chini ufikiri halafu utoe mawazo yako hapa.
No comments:
Post a Comment
Asante kwa ku Comment yako ujumbe wako ni muhimu