SHIRIKA LA NDEGE
BINAFSI
Ndugu
mdau wa Buberwa Robert Blog,
Najaribu
kukupa kitu ambacho nakiwaza kichwani kwangu, kichwa change kimejaa mambo mengi
sana ambayo huwa nashindwa kuelewa, je hatuna watu wanao waza, wapo lakini ni
mambo magumu, mfumo wetu ni wa kusubiri serikali ifanye nasi tukosoe au
kushangilia pale jambo linapoenda kinyume na matarajio ya wananchi?
Leo
naomba niongelee kuhusu usafiri wa anga kwa kuanzisha kampuni yetu ya usafiri
wa anga itakayoitwa vyovyote wadau watakavyoamua, shirika litakalokuwa na
malengo ya kusafirisha abiria ndani ya Tanzania yaani mikoa yote, nje ya
Tanzania ikiwa na maana ya Afrika nzima na dunia. Tutafanyaje hadi tuweze kutokea hadi nje huko
duniani, ni mipango ya shirika litaloongozwa na wasomi wenye ueledi wa hali ya
juu na si wale ambao kila kitu kwao hakiwezekani. Ikiwa wenzetu wanaweza kwa nini sisi
tushindwe ikiwa tuna saa 24 wote, miaka sawa, tunavuta hewa moja, dunia ni moja
ambayo iko katika mfano wa duara, wao dunia yao haipo flat kwanini tushindwe?
Ndugu
mdau unayesoma hapa, ninataka utoe mawazo ambayo yatakuwa na tija kwako,
kwangu, kwa Yule na wale na Tanzania nzima, leo naongea hili kama ndoto lakini
siku likitimia kila mmoja atajisifia, leo hii tunasoma lakini masomo yetu
yanatutengeneza tuwe nani, kwanini hatuwi wabunifu, na ubunifu wenyewe uwe wa
kuzalisha ajira, kuzalisha fedha, kuzalisha utaalamu na si kusoma na kuzurura
na bajasha ukitegemea kuajiriwa, mimi nasema ni aibu kwa msomi mwenye elimu ya
juu kutembea na bahasha eti anatafuta ajira, hiyo elimu yako unataka uitumie
kwa kufungwa kwa kupangiwa muda wa kazini, mpango kazi usio na tija kwako na
familia yako, unawafaidisha waajiri tu ndani ya miaka yote unayofanya kazi.
Leo
nakuja na mada ya kufikirika lakini inayowezekana ikitendewa kazi, na si
kuidharau na kuona huyu jamaa anawaza nini mbona hiki kitu kigumu, unajua
maendeleo yanaletwa na wewe pale unapowaza maendeleo, na si kulalamikia
maendeleo yaletwe na mwingine.
Hivi
umeshawahi kuwaza kununua ndege labda aina ya Boeing 777 ambayo inauzwa dola za
kimarekani 76 milioni, bei ya chini ambapo tunaweza kuwaza kuchanga kwa kiwango
chetu na kuchukua mikopo pia ikiwezekana ili tuweze kuanzisha kampuni yenye
hata ndege 10 kwanza, ikiwa ndege 2 kubwa za kutoka nje ya nchi jirani, na
ndege 8 ndogo za abiria kuanzia 6 hadi 60 zitakazokuwa zinakwenda mikoani kila
siku kwa bei nafuu?
Wengi
wetu tunasomesha watoto, sisi tumeshafubaa, kwanini tusitengeneze kampuni kubwa
ya usafirishaji wa anga, kampuni ambayo itaaminika ndani na nje ya nchi kwa
huduma bora? Huwa hatuna mawazo haya
zaidi ya kutaka kupinduana kisiasa tu kila siku? Nina hakika kama tuna hasira na maendeleo
basi tunaweza tengeneza ajira za vijana walio wengi tena watoto wetu wenyewe na
sio wageni ambao watakuja kuchukua hadi senti ya mwisho, sikatai kuna sehemu lazima wataalamu wan je
waingie lakini waingie kwa mkataba ambao utatutengenezea watanzania wataalamu
kama ao katika vyuo vikuu vya duniani huko ambavyo vitawaamini wasomi wetu.
Kuna
huduma nyingi za anga, kama kusafirisha abiria, kusafirisha mizigo, kusafirisha
wagonjwa, kuzima moto, kuchukua picha, huduma za kilimo, huduma za hali ya hewa
na mambo mengine ambayo yanawezekana.
Kila
mara huwa naongelea suala la kujiunga na kutengeneza kitu kikubwa chenye maana
kwa wananchi hiki kitu kama kweli tutafunga macho na kweli kuamua kuwekeza
tunaweza kufanya jambo kubwa sana katika nchi hii, Shirika letu litatakiwa kuwa na kiwango
kisichopungua dola za kimarekani zaidi ya 10 trilioni ili kuweza kuanza angalau
kwa ndege chache ndogo na kubwa.
Najua
mdau unayesoma hapa una maswali mengi kuhusu jambo hili lakini kama tutakaa na
kujadili na wataalamu wakaanza kuandaa Business Plan na tukafanikiwa kuanza
kuchanga na mambo mengine ninaamini hili shirika linaweza kuanza na kila mmoja
wetu akaja kujisifia sana huko mbele ya safari.
Tutatakiwa kujua, faida, hasara kwa upande wa fedha, usafirishaji,
abiria au wateja kwa kuingia katika biashara sio kwa kulikatalia kichwani.
Siku
zote ukijipa majukumu mazito utafanikiwa, lakini ukiyaachia majukumu kwa wengine
huwezi kuendelea kwa kuwa maendeleo yanakutegemea wewe ili yaendelee. Kumbuka wenye mawazo si lazima wawe wasomi,
na watendaji si lazima wawe wenye fedha, bali kila mmoja anamtegemea mwenzake
kwa jambo moja ama lingine. Tushirikiane
ili tuijenge Tanzania yenye mafanikio na si malalamiko
Hivi
naeleweka?
No comments:
Post a Comment
Asante kwa ku Comment yako ujumbe wako ni muhimu