Mtu yeyote ambaye
anapata walau mlo mmoja kwa siku na kupitisha kati ya siku moja au tatu bila
kupata choo, ana tatizo la kukosa choo (Constipation).
NINI KINASABABISHA KUKOSA CHOO?
·
Kukosa mlo
kamili. Kama vile kula vyakula vyenye
kiwango kikubwa cha wanga na mafuta.
·
Kula vyakula
vilivyokobolewa na vilivyo changanywa na madawa ili visiharibike.
·
Mifumo hatarishi
ya maisha kama vile matumizi ya sigara na pombe uliokithiri.
·
Ukosefu wa
kiwango cha kutosha cha mbogamboga na matunda katika mlo, ila nakushauri ule
matunda saa moja au mbili kabla ya mlo au saa moja au mbili baada ya mlo.
·
Maji yasiyo
salama.
·
Kuvuta hewa
chafu.
·
Na nyingine
nyingi zinazosababishwa na maisha yanayoendeshwa na mabadiliko ya sayansi na
teknolojia.
ATHARI ZA KUKOSA CHOO
·
Chakula
kutomeng’enywa (kusagwa) vizuri.
·
Maumivu makali
wakati wa kupata choo.
·
Uchafu uliokaa
kwa muda mrefu kugeuka sumu.
·
Bakteria wenye
madhara kuzaliwa na kuathiri utumbo mpana na viungo vingine mwilini.
NI MAGONJWA GANI SUGU YANAYOWEZA KUSABABISHWA?
·
Saratani ya
utumbo mpana (colon cancer)
·
Presha
·
Kuongeza uzito
(obesity)
·
Tumbo kujaa gesi
·
Magonjwa ya ini
·
Figo kushindwa
kufanya kazi vizuri
·
Maginjwa ya
ngozi
·
Kukakamaa kwa
mishipa ya damu
·
Kisukari
·
Magonjwa ya moyo
·
Na matatizo
mengine mengi
NI NINI SULUHISHO SAHIHI LA TATIZO LA KUKOSA CHOO?
Ondoa mgandamano wote
wa taka katika utumbo mpana ukiuacha ikiwa msafi na wenye afya zaidi.
FAIDA YA KUONDOA MGANDAMANO
·
Ni njia haraka
na salama kwa afya yako
·
Inazuia saratani
ya utumbo mpana (colon cancer) na madhara mengine kiafya (coprostasis)
·
Tatizo la kukosa
choo utakuwa umelimaliza
·
Utapunguza uzito
uliozidi
·
Utaifanya ngozi
iwe yenye afya, nyororo na muonekano mzuri
Samahani
kwa kusema hivi, lakini ni ukweli uliowazi kuwa watanzania tuna aibu sana ya kuingia
maliwato huku tunaangaliwa na watu wengine.
Hii ni mbaya sana kwa kuwa pale unapobana haja kubwa ukasema nitaenda
baadaye unatengeneza pochi katika utumbo, chunguza mara ngapi umejibana kuanzia
wakati huo hadi umri huo ulio nao, ni vipochi vingapi umetengeneza, una
takataka kiasi gani katika utumbo mpana?
Utafanya
mazoezi, utapunguza kula utakunywa baadhi ya dawa za kupunguza mafuta mwilini
lakini utabaki na kitambi kikubwa unajua kwanini? Kwa sababu ya vipochi ulivyovitengeneza kwa
kubana choo.
Pili
hata ukiingia maliwato unakimbiakimbia likitoka tonge moja basi umeshanawa
umekimbia, ni hatari sana kufanya hivyo, unatakiwa ukae kuanzia dakika 10 na
kuendelea ili kila kilichokuwa kinatakiwa kutoka kitoke kwa wakati huo.
Tatu,
usilazimishe au usijikamue ili kutoa unachohisi kipo unachotakiwa kufanya
hakikisha umejiachia na kuiacha misuli ijifungue yenyewe kwa wastani wake ili
kilichopo kitoke kama kinavyotakiwa.
Ikilazimisha ndio yale yale kubakiza vipochi kila siku.
Kwa
kweli wengi wetu tunakosea mambo mengi sana katika maisha yetu, kuanzia kula,
kulala, kuvaa, kujisaidia haya yote ukifuatilia utakuta tunajitengenezea
magonjwa bila kujua.
JE UTAJUA KUWA RANGI YA KINYESI, HARUFU YA KINYESI
VINAWEZA KUKUONESHA UNA UGONJWA GANI AU BAKTERIA KIWANGO GANI?
JE UNAJUA KUWA MUUNDO AU SHAPE YA KINYESI INAWEZA
KUKUTAMBULISHA UNA SHIDA GANI
·
Kama kinyesi
chako ni kama ndizi uko sawa
·
Kama kinyesi
chako ni kama mbuzimbuzi kuna shida aidha ya maji hunywi ya kutosha
·
Kama kinyesi
kina tawanyika kama mafuta kuna shida
·
Kikiwa hakina
shape pia ni shida
·
Kinyesi kikiwa
kinashika katika sinki la choo ni shida kubwa sana hiyo pia
·
Kinyesi kikiwa
na harufu mbaya kali ni tatizo kubwa pia
Hili ni somo nalo tutalisoma kwa kifupi naomba
endelea kuingia katika blog hii kila mara kila siku
Kama
utaona una matatizo au tatizo lolote katika haya niliyotaja hapa, hasa kukosa
choo, vidonda vya tumbo, gesi tumboni, manyama uzembe, matatizo ya ngozi, basi
wasiliana name ili tujue la kufanya.
Kwa
mawazo zaidi wasiliana name nitakuelekeza cha kufanya na matatizo yako
yatatuliwa.
No comments:
Post a Comment
Asante kwa ku Comment yako ujumbe wako ni muhimu