Social Icons

Friday, 31 January 2014

KWA WAJASILIAMALI NA WANAOTARAJIA KUINGIA HUKO: HUU NDIO UFUGAJI WA KUKU WENYE TIJA , JIFUNZE HAPA


UFUGAJI WA KUKU

Mdau wa blog ya hii.
Wengi wetu tunafuga kuku pasi na malengo, nimekaa chini na nikaona uchoyo ni jambo moja baya sana linalotuumiza sana watanzania katika maendeleo ya kila jambo. (Hasa uchoyo wa mawazo, tunalaumu mno hatutoi mawazo yenye tija)
Leo naongelea kuhusu ufugaji wa kuku, hasa kuku wa kienyeji ufugaji wenye tija.

Kuku hawa ni rahisi sana kuwafuga lakini ni wagumu sana kama hutokuwa makini na kama huna malengo na ufugaji wako.  Wengi wetu tunafuga tu huku tukiwa na matarajio makubwa ya mafanikio.  Unajidanganya ndugu yangu, huwezi kutegemea kitu ambacho hukipendi na hukigharamii.  Kuku wanatakiwa kula, kuku wanatakiwa kunywa, kuku wanatakiwa kupata huduma za dawa, kuku wanataka kulala sehemu nzuri na safi, yenye hewa, wanapopendwa, wanapojaliwa, kuku wanahisia kama viumbe wengine huwa wanapenda wakiwa na shida uwaangalie kama unavyoangalia kitu kingine chenye uhai na uwasaidie, lakini ukiwa mkaidi kwao nao watakuletea ukaidi.  Haya ni maneno huwa naambiwa na mama yangu mzazi bi Paulina, huwa anawaangalia kuku wangu na anasema hawa kuku wana shida lakini huwaelewi, sasa nimeanza kumuelewa na ndio maana nataka nikupe elimu hii nawe uweze kufaidika.

ONDOA UCHOYO KWANZA

Kama umeamua kufuga kweli basi fanya haya, usiwe bahili wa muda kwa kuku wako, usiwe bahili wa vitu vifuatavyo;
a.       Fedha za kununulia chakula
b.      Fedha za dawa na daktari
c.       Fedha kwaajili ya kununua mboga za majani au ufanye kilimo cha mboga za majani ili uwalishe
d.      Fedha kwaajili ya ulinzi wa kuku wako
e.       Fedha kwa mtunzaji wa kuku wako
f.       Fedha za usafirishaji kwenda kwa wateja wako, au katika manunuzi ya kuku wageni




Lakini kuna jambo kubwa zaidi, umoja kati yako wewe na wafugaji wenzako.
Na hii leo ndio mada yangu kuu.
Umoja wa wafugaji katika eneo hilo ulilopo, ndio nguzo kuu ya kupata kipato kikubwa zaidi na kuwa na soko kubwa zaidi mwaka mzima na miaka yote na hakuna mtu anatakayekosa huduma ya kuuziwa kuku au mayai katika eneo lenu ikiwa mtakuwa wamoja kwa ufugaji wa kuku.
LENGO MOJA NA MOYO MMOJA
Ni vigumu sana kwa watu zaidi ya 100 kuwa na lengo moja kwa miaka zaidi ya 10, lakini kama mtaamua na mkaona faida yake inawezekana tena kwa 100%.  Naongea haya kwa kuwa naona kabisa ili ufanikiwe kuwa kama unataka kuku 10,000 kwa kipindi kifupi ni ngumu lakini wafugaji 30 mkiunda kikundi na mkachangishana labda shilingi 500,000 kwa kila mmoja mtapata shilingi za kitanzania 15,000,000.  Mkiamua sasa mjenge banda la shilingi 3,000,000 zitabaki 12,000,000. Na mkinunua chakula cha shilingi 3,000,000 zitabaki milioni 9,000,000.  Wengi wa wauzaji wa kuku huuza kuku waliochanjwa hivyo unaweza kukaa na kuku wale kwa miezi mitatu zaidi wakiwa wako vizuri bila kuugua. Nunueni kuku kwa shilingi 1,600, leo nakupa siri kama ulikuwa hujui nipigie simu nitakuambia vizuri wapi pa kununulia na utashangaa utakuja kuwa na kuku hadi ulie. Katika milioni 9,000,000 zilizobaki nunua kuku wa shilingi 5,000,000 kwa kila mmoja kumnunua kwa shilingi 1,600 utapata kuku wangapi?

Utapata kuku 3,125.  Kuku hawa utawanunua wakiwa na umri wa miezi mitatu na nusu, hivyo utawakuza kwa miezi miwili na nusu wataanza kutaga.  Lakini kama mtataka kuwa na kuku wengi zaidi kwa muda wa miezi 6 mnaweza kuwa kundi lenu la watu 30 mkawa mnachangishana 200,000 kila mmoja ina maana kila mwezi mtapata shilingi 6,000,000 x 6 = 36,000,000.
36,000,000/1,600 = 22,500
Kundi litapata kuku 22,500 ina maana kama kuku mmoja baada ya miezi minne atauza kwa shilingi 10,000 kwa kuku 22,500 kikundi kitapata shilingi 225,000,000.
Kwa maana hii kikundi kitakuwa kimepata faida ya shilingi;
225,000,000 – 36,000,000 = 224,964,000
224,964,000 – 50,000,000 = 174,964,000
Hiyo hesabu ni makadirio na matumizi ya kilichopatikana ilitumika 36,000,000 kununua kuku 22,500 wakauzwa kwa shilingi 10,000 kwa kila mmoja ikapatikana shilingi 225,000,000 tunatoa fedha ya manunuzi iliyokuwa shilingi 36,000,000 hivyo itabaki shilingi 224,964,000 katika pato hilo la 224,964,000 toa 50,000,000 ya vyakula, maji, mlinzi, mhudumu, umeme na maji utabaki na shilingi 174,964,000 (weka hasara ya kuku wengine kufa) faida itakuwa 100,000,000
Hii inaweza kufanya kila mwanachama wa kikundi akawa na faida ya shilingi 3,333,333.30 ambapo mkiamua kujiwekea malengo ya kuuza kuku kwa mizunguko 1,000 kila mwanakikundi atakuwa na faida ya shilingi 333,333,300 na hii inawezekana sana kama kundi lina nia na linaupeo na si kulalamika kila wakati.  Tatizo letu watanzania ni walalamishi sana sio wote ila asilimia kubwa ni walalamishi.  Nina hakika kundi hili linaweza kujikwamua kwa kuku tu bila kujichanganya na jambo lingine.  Kundi likijipa miaka mitano ya kufanya biashara hii kwa nguvu na nia itakuwa mfano wa kuigwa.
Kumbuka kuna kundi la kwanza la kuku 3,125 ambapo kuna shilingi 4,000,000 ilibaki benki kama kilinda benki, kikundi hiki kwa mahesabu yale yale kina uwezo wa kutengeneza shilingi  na shilingi za mamilioni.  Ila sasa huku itazitengeneza kwa kuzalisha mayai ya kuku wa kienyeji.

MAYAI YA KIENYEJI
Ikiwa kuku  3,125 majogoo yatakuwa 1,125 na majike 2,000 basi una uhakika wa kuwa na trei 66 kwa siku.  Chukulia mfano siku 7 za wiki unachukua mayai manne tu kwa wiki utapata mayai 16 kwa kuku hii inamaana utapata mayai 32,000 kwa mwezi ambayo ni trei 1,066.  Trei moja ya mayai ikiuzwa shilingi 12,000.

1,066 x 12,000 = 12,792,000 kwa mwezi
12,792,000 x 12 = 153,504,000 kwa mwaka
Kwa maana hiyo mayai yanaweza kuingiza shilingi 153,504,000 ukitoa gharama za usafirishaji na mhudumu mnaweza ingiza 100,000,000 kwa kuuza mayai ya kienyeji pekee.

Kwanini tusijiunge tukafanya shughuli hii?
Unasubiri nini?
Unataka kuona nimetajirika kwanza ndio na wewe uhamasike?
Usiwe mchoyo njoo tujiunge tukuze kipato kwa biashara hii niliyokupa sasa hivi


MBOLE YA KUKU
Kinyesi cha kuku ni mbolea nzuri sana kwa wakulima, kwa idadi ya kuku iliyopo katika kikundi na inayoendelea kuwepo kila mfuko wa mbolea ya kuku inauzwa shilingi 2,000.  Ikiwa kikundi kitakuwa na mifuko isiyopungua 2,000 basi kikundi hakitakosa shilingi 4,000,000 iliyotokana na mbolea.

Mifumo mingine utaweza kuipata tukiwa wote katika kikundi na tutaibuni zaidi na zaidi.  Kwa leo niishie hapa, nashukuru kwa kusoma wazo langu, ninaomba mawazo yako na tuyafanyie kazi ili tujikwamue kiuchumi.
Mawasiliano yangu yanapatikana katika blog yangu moja kwa moja karibu, ila bahati mbaya simu yangu namba +255765903379 imepata shida kidogo sitakuwepo hewani kwa muda, iwe katika WhatsApp, Instagram naomba radhi kwa usumbufu ila namba nyingine zote nipo hewani

Wednesday, 29 January 2014

FAHAMU BIASHARA NZURI YA BATA MZINGA, SOMA HAPA


BATAMZINGA

Bata Mzinga ni biashara nzuri sana ambayo watu wengi hatuitilii maanani sana.  Soko la Bata Mzinga ni kubwa sana katika Supermarkets.

                            
Wengi watahoji nitafugia wapi! Hautakuwa una shida ya hela ndugu yangu, lakini sikulaumu sana kwa kuwa mfumo wa sisi hasa watanzania ni kuajiriwa, na ajira zetu hizi za kupata mwisho wa mwezi kiasi kidogo cha hela na kuridhika, huwa kinatudanganya sana.  Wengi wetu hujiingiza katika makundi ya udanganyifu kwa kuwa tunatafuta kipato cha ziada kwa njia isiyo halali, na mwisho wa siku ajira zetu sasa zina dhambi, dhambi ya rushwa, kutokuaminika, kuharibiana ajira.  Hii yote ni dhambi tu, hatutaki kushirikiana ili kuweza kufanya kazi kwa bidii na kukuza kipato chetu na kufanya kazi za umma kwa maslahi binafsi, na maslahi ya umma.
Sio mada yangu hii leo lakini naomba tujue baadhi ya sababu zinazojenga ukanjanja kazini.  Hatujipangi kikamilifu, tunacheza na majukwaa (tunataka kuonekana na jamii tuna uwezo kumbe si kweli)
Bata Mzinga ni bata anayefugwa nyumbani, na ana uwezo wa kukua hadi kufikia kilo 15, ni
pambo la nyumba pia.

Kwanini namuongelea Bata Mzinga leo, nimegundua kila ninapoenda katika Super Markets kubwa nakuta nyama ya bata hawa inauzwa na tena bei kubwa tu, mfano mimi nilinunua kifaranga cha bata mzinga kwa shilingi 25,000 walikuwa watano ambayo ni sawa na shilingi 125,000.
Kwa wale wanaojua kilo moja ya bata mzinga inauzwa kuanzia shilingi 10,000 na bata mzinga ana kilo 15 ni sawa na shilingi 150,000 hivi huoni kuwa huyu muuzaji wa kilo moja moja anafaida kubwa sana kuliko wewe mkulima?
Bata mzinga mmoja mwenye kilo 12 kwa jike na kilo 15 kwa dume anauzwa hivi;
Bata mzinga jike ni shilingi 60,000
Bata mzinga dume ni shilingi 70,000
Mfano una bata mzinga 2,000, majike 1,000 na madume 1,000 unajua utakuwa una miliki shilingi ngapi?
Ukiwa na majike 1,000 wenye thamani ya shilingi 60,000 = 60,000,000
Ukiwa na madume 1,000 wenye thamani ya shilingi 70,000 = 70,000,000
                                                                                                                       
Mfano ukijiingiza katika biashara hii kwa kununua bata mzinga wadogo 40 kwa shilingi 25,000 kwa kila mmoja unaweza kupata majike 25 na madume 15 kwanza ili uanze kutengeneza kizazi cha kufuga kwanza.  Chukulia mfano jike moja likitotoa vifaranga 10 x 25 = 250.  Fanya kila bata mzinga atotoe mizunguko mitano itakuwa 250 x 5 = 1,250

Sasa chukua hao watoto 1,250 nao wawe madume nusu na majike nusu 625 x 10 = 6,250.  Chukua idadi ya kwanza 40 + 250 + 1,250 + 6,250 = 7,790 unaona wanavyoongezeka kutoka 40 hadi sasa una bata mzinga 7,790 tayari hapa wewe ni milionea hizi ni sawa na shilingi 467,400,000 unazo ndani.
Bata mzinga 7,790 ukiwagawa madume na majike nusu kwa nusu utapata majike 3,895 chukua kila bata mzinga atotoe vifaranga 10 kila mmoja utapata bata mzinga 38,950

UUZAJI VIFARANGA
Hawa bata mzinga 38,950 unaweza kuuza kama vifaranga, na kila kifaranga utakiuza kwa shilingi 25,000.  38,950 x 25,000 = 973,750,000 hii ni fedha taslimu utaipata kwa kuuza vifaranga.


 
Katika miaka kumi ya ufugaji wako wa bata mzinga unaweza kujikuta unakuwa bilionea kama ukiwa makini na mwenye nia kweli ya kuzitafuta pesa kwa kuwafuga hawa bata. 
Leo tumeanza na bata mzinga 40 lakini tunamaliza na bata mzinga 46,740 wastani wa bata mzinga 50,000.
Kazi yangu ni kukupa changamoto mdau mwenzangu katika kutengeneza maisha ya ufugaji na fedha.  Unaweza kustaafu kazi ya kuajiriwa lakini ukaanza ufugaji na ukatengeneza hela nyingi zaidi, usikate tama.  Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, alianza madaraka mwaka 2005 jana tu tulimpigia kura kwa shangwe na vigelegele, kumbuka 2010 tena tumempigia kura na sasa amebakiza mwaka mmoja tu wa madaraka yake, je huoni kuwa jana tu imeshageuka leo? Hujachelewa bado kwa mwaka huu wa madaraka yake na mwezi huu Januari, 2014 badilika anza ufugaji nenda na malengo kama haya, nakuhakikishia nitakutafutia masoko pia, na nitakutangaza kwa moyo wangu wote. Sijui atakayenisaidia mbele ya safari.  Ila wewe utakayefuata haya ninayokuambia na ukafanikiwa usinisahau katika ufalme wako, hata kama sitakuwepo basi waangalie hata wanangu.

Ushauri wangu kwako usitake makubwa haraka nimekupa mfano wa Raisi wan chi ili uone kuwa miaka 10 ni mingi kuitaja, lakini ni michache ukibung’aa huku unangoja maisha bora na elimu yako unapanda jukwaani unalalamika pamoja na asiyena elimu, ni wakati sasa wakutoa vilivyo kichwani na kuviweka katika maandishi na vifanyiwe kazi.
Tuwasiliane kwa kupeana mawazo
Maoni yako ni Muhimu sana 

Tuesday, 28 January 2014

SOMO MUHIMU LA LEO: FAHAMU JUU YA BIASHARA YA MTANDAO , JIKOMBOE SASA NA WEWE KUANZA BIASHARA HIYO, SOMA HAPA



BIASHARA YA MTANDAO:
Biashara ya mtandao ni biashara inayozaa na kuzalisha, ni biashara ya kuambiwa, kukubali, kutumia, na kuwaambia wengine, ili nao wafanye kama ulivyofanya wewe yaani uwaambie, wakubali, watumie nao wawaambie wengine. (DUPLICATION)
Leo nazungumzia biashara ya mtandao kwa kuwa watanzania wengi kama bado hawajaielewa hivi na walioielewa kama wanapotosha hivi baadhi yao.


Utakuta unatoa darasa au unamuelezea mtu kuhusu biashara ya mtandao anakuja si ile kama kampuni Fulani, huo ni unafiki sio kujua huko, kama uliskia kaa kimya mbona hukuanza wewe.  Msikilize anayetoa mada tena katika wakati na sehemu inayoeleweka, kwanini naongea haya, kwa kuwa utakuta wengi wa watu hawa kabla hujaendelea anaanza kuelezea kampuni ingine na kuanza kuiponda au kuisifia, ingawa wengi utasikia ya nchi gani hiyo, hamna lolote mimi nimeshatumia sana.

Biashara ya mtando ilianzishwamiaka ya 1960s huko Marekani na mamilionea wengi wa marekani walianza kushika milioni yao ya kwanza kwa kupitia Biashara hii ya mtandao.

Kwa hapa kwetu Tanzania makampuni yanazidi kuja mengi na biashara hiyo inazidi kushika kasi kwa nguvu kutokana na wengi wanavyoonja mafanikio.
ukisikiliza watu wanavyoifanya biashara hii utakata tamaa na kuitwa machinga lakini kiuhakika na ukweli biashara hii haipaswi ubebe bidhaa uzunguke nazo kama machinga.  Wengi tumeshindwa kuelewa biashara hii na ndio maana mtu akifanya baada ya miezi mitatu au minne anahisi haoni mafanikio mwisho anaamua kuacha na kusema biashara hailipi, wakati anafanya biashara hii kimakosa
Jinsi ya kufanya hii biashara ni kama nilivyosema ambiwa, kubali, tumia, muambie na mwingine, akubali, atumie naye amuambie na mwingine.
Ili ufanikiwe katika biashara hii ni lazima kwanza uijue kampuni, mwenye kampuni, bidhaa zake, na mfumo wa biashara yenyewe.  Biashara hii ni ngumu sana lakini wagumu ndio watakao baki.  Tuna ushahidi wa wafanyabiashara wengi wa biashara hii ya mtandao ambao wanapata kipato kikubwa mwisho wa mwezi, na mwisho wa mwaka, wapo wanaopata hadi shilingi milioni 10 kwa mwezi, na mwisho wa mwaka wanapata zaidi ya shilingi milioni mia mbili na zaidi (TSHS. 10,000,000 hadi 200,000,000) kama ulikuwa hujui jua kuanzia leo.  Biashara hii ukiisikiliza unaweza kwenda kukopa mabilioni ya shilingi ili uje upate yale yote unayoambiwa katika kampuni ile, ni kweli wayasemayo yanapatikana hakuna mjadala, hakuna tapeli hata kampuni moja katika zilizopo Tanzania, tatizo ni wafanyabiashara wameelewa muundo wa biashara hiyo? 

Wanajua jinsi ya kuwatafuta wateja? Je kuna idadi gani ya watanzania walio na afya njema, kuna idadi gani ya watanzania wanaoumwa, na je kuna idadi gani ya watanzania wanaoumwa huku hawatambui kama wanaumwa.
Angalia taarifa hii ilitoka mwaka jana katikati yaani 2013, inasema hivi katika watu bilioni saba (7,000,000,000) dunia 5% wana afya njema nao wana umri wa miaka kuanzia 0 hadi 5 je wewe unayesoma umo humu kwenye hili kundi?.  20% ni wagonjwa waliolazwa Muhimbili, na  Hospitali nyingine unazozijua ndani na nje ya nchi pia na wale wanaotumia dawa kwa kutambulika.  Na 75% ni wagonjwa watarajiwa au wanaotembea na ugonjwa pasi na kujua na ndio maana utakuta wengi wetu tuna kufa ghafla maana tuna magonjwa huku tunatembea na huku akili zetu nafsi zetu zikitundanganya kuwa ni wazima wa afya.  Nikuulize swali! Lini ulisikia kitu kama radi kimepiga upande wa kushoto ukashtuka ukakimbilia hospitali?  Na lini gari yako imelia kitu mvunguni tiii au umesikia mvumo huuelewi ukakimbia kwa fundi? Acha unafiki jibu ukweli.  

Huo ukweli wako ndio utakuponya.
Kama nilivyosema biashara hii ilianza miaka ya 60, sisi ndio inaingia sasa Tanzania ndio maana tunashtuka hatuzijui vizuri kampuni hizi wala biashara hii, na bahati mbaya biashara hii ya mtandao imekuja Tanzania na makampuni ya virutubisho mengi au yote kuliko ya vifaa kama sufuria, umeme na kadhalika.  Wenzetu walio endelea hukimbilia sana biashara hii kwa kuwa inalipa vizuri sana, huku kwetu hasa Tanzania tunaikimbia kwa kuwa ni ya kujituma.

Biashara ya mtandao inajenga asikuambie mtu, unajua mambo mengi kuliko unavyodhani, wala usitangulize dharau kuwa hawa ni wamachinga sijui wanaongea sana hapana, tena biashara ya mtandao hutakiwi kuwa muongeaji sana, unatakiwa kuwa mtumiaji sana wa bidhaa ili wengine waone mabadiliko yako nao watamani kutumia bidhaa unazotumia, ili nao wawe kama wewe.

KOSA KUBWA TUNALOFANYA WAFANYABIASHARA WA MTANDAO
Unaposikia au unapoitwa katika kampuni ngeni au wewe ni mgeni katika kampuni ile basi kuna wale wenyeji wanaokujua na kukuita pale basi hukuita kichwa, jembe kwa kuwa wanaamini ukiingia utawabuzuta watu wajiunge na ile kampuni kwa kuwadanganya mambo yasiyo ya kweli na kweli ili waingie na mwisho wakiingia hawaoni ulicho maanisha kwa kuwa hayo uliyosema si ya kuonekana leo ni hadi miaka mitatu hadi mitano, na kosa lingine ni kitendo cha kuanza kupiga hesabu kichwani eheeee nimeambiwa kuna dawa ya kisukari nina shangazi ana kisukari, mjomba ana kisukari, jirani ana kisukari, fulani ana matatizo ya hedhi, mama fulani ni mnene sana, mama ndimu, ana vidonda vya tumbo, bi mkora ana pressure, shekiangio ana tatizo la ngozi baaasi watakoma naenda kila mmoja anipe shilingi laki nne nimpe full dozi, sasa utakuta mwana mtandao anaenda kwa wateja wenye hela ili apate bonus, na points za mwezi bila kuangalia biashara hii haitaki wagonjwa kwa asilimia kubwa, biashara hii inataka mtu atumie virutubisho hivi kwa kuwa vyakula tunavyokula, maji na juice na pombe tunazokunywa zina sumu, pia dawa karibu 90% zina kemikali hivyo tunatakiwa kutumia hivi virutubisho ili kuondoa kemikali hizo.

Sasa hivi kila chakula kila tunda, kila mboga inawekwa dawa, au mbolea zina dawa, hivyo ni vyema kujifunza vyema bidhaa hizo ili kuweza kutafuta wateja wa kujiunga na kuzitumia kwa mafanikio, tatizo sio kampuni na wala tatizo si nchi tatizo ni sisi wasambazaji, tukitulia na kujifunza vizuri tutaisaidia sana jamii.

Hospitalini ni sehemu ya kikinga maradhi, lakini sasa hivi ni kinyume, hospitalini ni sehemu ya kutibu magonjwa tena yaliyoshindikana, elimu hizi ambazo zinatolewa na makampuni ya virutubisho ilitakiwa itolewe na manesi na madaktari ili watu wasifikie hatua ya kuumwa, figo, kuto kupata choo, moyo, macho, ngozi, kutokupata hedhi, ulaji bora wa chakula bora, unywaji wa maji, unywaji wa sharubati, utumiaji wa mboga za majani na kadhalika. Haya yote yanatakiwa kufanywa na hospitali, lakini pongezi kwa wafanyabiashara wa biashara ya mtandao wanafanya kazi kubwa sana kuelimisha jamii, ingawa jamii yenyewe nayo kuelewa ni kazi sana, lakini naamini wataelewa tu.

BIASHARA YA MTANDAO INAIINGIZIA SANA SERIKALI MAPATO
Kama ulikuwa hujui basi biashara ya mtandao inaiingizia sana serikali mapato, maana kampuni inapoingia nchini inafuata taratibu zote za kisheria, za ulipaji kodi na inapewa TIN namba na inaingia katika usajili wa ulipaji wa kodi kisheria.  Ukitaka kujua hili zaidi nitafute nikupeleke ukaone.

WAFANYABIASHARA YA MTANDAO WANAKOPESHEKA
Unapojiunga katika kampuni yoyote ya biashara ya mtandao unajisajili na kuweka vielelezo vyako vyote katika fomu, na pia kampuni inakutambua kuanzia katika nchi yako hadi dunia nzima ambapo kampuni hiyo ipo, kwa kuwa unapofikia cheo fulani basi kuna kamisheni unapata kutokana na cheo chako na wale wenzako mlio katika cheo kile katika dunia nzima, hivyo gawio la pato la mwezi huo linagawiwa kwa ninyi mameneja wote duniani.  Vile vile unapopanda cheo kimoja kwenda cheo kingine kampuni itakutambua na kukupa cheo chako na dunia nzima itakutambua kwa kufikia hatua hiyo.  Sasa nauliza mabenki yaliyopo hapa Tanzania kuna siku mlishawaza kuwafuata wafanyabiashara wa mtandao na kupata darasa kuhusu biashara hii inayoingiza mamilioni ya shilingi hapa nchini kila siku? Je ikiwa sisi wafanya biashara wa mtandao tunatambulika nje ya Tanzania kwa nini benki iliyopo Tanzania isinitambue? Naomba sana watu wa benki kama mnataka faida kubwa nioneni mimi niwaoneshe wapi mnalosa wateja wengi wenye pesa nyingi na wanaokopesheka na wenye uwezo wa kulipa halafu ninyi hamuwafuatilii.  Biashara yoyote ambayo mfanyabiashara anaweza kupata kuanzia shilingi 100,000 nadhani anakopoesheka bila matatizo kikubwa ni kufuata taratibu, kanuni na sheria za mikopo.
Naamini ikiwa benki zitatutambua na kutuamini tunaweza kukopa na kufanya biashara zetu na kurejesha mikopo kwa wakati, kikubwa kinachotakiwa ni kupeana elimu tu.
Imani yangu wanamtandao tukijiunga vikundi vya watu kuanzia 30 kama vicoba tunaweza kupata mikopo mikubwa na kufanya mambo makubwa sana katika biashara hii.

Nakuomba mdau unayesoma hapa kama utakuwa hujaelewa na una swali usisite kunipigia simu, kutuma sms, au email ambazo zinaonekana katika mawasiliano hapo ili tupeane mawazo zaidi.
Hii ndio ajira ya karne ya 21, inakupa uhuru wa muda, uhuru wa pesa, uhuru wa kustaafu unavyotaka.
Pesa zipo hapa!

Monday, 27 January 2014

JE UNAJUA KUWA MTO MSIMBAZI, UKITUMIKA VEMA UTAWEZA KUPUNGUZA FOLENI JIJINI DAR ES SALAAM?



Mto Msimbazi ni mto mkubwa sana ambao unaweza kutumika kwa usafiri, moja ya kupunguza adha ya foleni barabarani ni kuutumia mto msimbazi kwa usafiri.

kuanzia Salender Bridge, Muhimbili, Jangwani hadi Vingunguti, na sehemu nyingine ulipopita.  Wale watengenezaji plan za miji wangeweza kufikiria jinsi ya kuufanya mto huu kuwa kivutia hapa Mkoani Dar es Salaam, kwa kushirikiana na wataalamu wengine.

Kila ninapo kaa na kuuangalia mto huu naona kuna kiasi kikubwa sana cha fedha mkoa kama mkoa na wananchi wake tunakosa, pia ni sehemu nzuri sana kwa kufanyia sehemu za burudani na mandhari nzuri zitakazo weza kuwavutia wawekezaji wa ndani zaidi na nje kuweza kufanya biashara katika maeneo yaliyopita kwa kuweka Hoteli, Migahawa, Nyumba za Kulala wageni, Sehemu za sherehe, Boti za kusafirishia abiria, mandhari nzuri za bustani.
Mimi sio mbunifu wa kuchora, wa kupamba lakini najua wapo wataalamu wanaoweza kutengeza ramani, picha, na jinsi ya kuyatengeneza maji yaweze kuwepo muda wote kwa kiwango kinachotakiwa ili boti ziweze kupita kwa miaka yote bila kuathirika na upungufu wa maji au takataka.  Nikiwa kama mtanzania ninayependa maendeleo ninaiona Tanzania tofauti kidogo na wenzangu kuna vitu vingi tunaweza kuvifanya katika mto huu wa Msimbazi na tukaweza kupata kipato kwa uvuvi, usafiri na mambo mengine mengi yatayobuniwa na kuwekwa pale, pia ni ajira kwa vijana, hapa ndipo pa kupatia ajira vijana wengi.

Nadhani wazo hili litakuwa na mantiki zaidi kama wataalamu wa Wizara husika na wananchi watatumia busara, hekima na utashi walio nao na kugombea mambo yasiyo na tija, tunaweza kwa silimia mia kuutumia mto huu kwa tija, na tusifikirie bonde la mto msimbazi tu kama bonde, tufikirie mto kama mto, maana sasa hivi mto ule hauonekani kwa kuwa umefunikwa na ujenzi wa vijijumba, majumba na kilimo, pia na kuwa sehemu kubwa ya utupaji taka.  Sidhani kama kazi hizi ndizo zinazotakiwa kufanyika katika mto huu.
Kuna wateja wengi sana ambao wanaweza kuutumia mto huu kuanzia mjini hadi vingunguti, kuna mabilioni ya shilingi tunaweza kuyapata kupitia mto huu, ni kiasi cha kubuni cha kufanya tu chenye tija.  Nimetoa mada moja inayosema jinsi ya kuyafuga maji tunaweza kuyafuga kwa kuyaingiza maji ya mvua katika mto huu kwa faida na kuweza kuutumia na kuingiza kipato kwa mkoa mzima.

Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wabunge, Madiwani, Mameya na Waziri wa Wizara zinazohusika mnaweza kukaa na wataalamu mkapanga la kufanya ili itokee mwisho wa siku kuwe na njia ya usafishaji wa kupitia mto Msimbazi, na msiwaze tu labda kuwe na uwazi wa kutengeneza sehemu ya michezo, tuutumie mto huu kwa tija.  Tusilifanye jambo hili kisiasa, tusiogope wananchi kulalamika kwa sasa, ila mwisho wa siku wataelewa namaanisha nini.  Watanzania tunatakiwa kuwa wabunifu na kuufanyia kazi ubunifu huu kwa manufaa ya nchi na wananchi na mwisho wa siku tufaidi wote.


Wana blog wa Buberwa Robert Blog! tutoe mawazo kwa michoro na picha ili tuijenge nchi yetu. 


Inawezekana kabisa Mto huu ukiboreshwa ukawa na faida kama baadhi ya mito hii hapa.






Monday, 20 January 2014

JALI NYUMBA YAKO:JIFUNZE! MAJI KUJENGEWA MATANKI MAKUBWA KWA MATUMIZI MENGINE


Ndugu mwana Blog wa Buberwa Robert kama ilivyo ada, tunajaribu kupeanaamawazo kuhusu maendeleo katika nchi yetu.
Katika fikira zangu za njozi, njozi ya maendeleo, nina ota kupatawataalamu (Engineers) ambao watabuni jinsi ya kuyafuga maji kutoka popote pale na kuyapeleka katika visima vikubwa sana ambavyo vinaweza kujengwa















kwa matumizi ya maji kwa wananchi, kwa wenzetu wa Zimamoto (Hydrants), kwa matumizi mengine mengi ambayo wadau tutajadili.
Wazo langu linakujaje kuna mitaro mingi sana inachimbwa katika mabarabara na mitaani, lakini mwisho wa siku ile mifereji na mitaro inaangukia sehemu ambazo kiukweli hazina faida zaidi ya kutengeneza mafuriko makubwa yatakayokuja kuumiza wanadamu, kwa kuwasoma, kujaa katika nyumba zao, kuvunja majumba, kuleta magonjwa. Pia kuleta ugomvi kati ya wananchi na serikali kwa kuwa mwisho wa siku wataambiwa wahame, mara wasogee.
Naomba kama kuna uwezekano mainjinia wakune vichwa vyao na waangalie ni jinsi gani maji ya mvua yote yana vunwa na kupelekwa katika visima vikubwa katika wilaya zote, na vitongoji ambavyo vitateuliwa kuwa ajili ya matumizi ya maji hayo badala ya kuyaacha haya maji yatiririke tu aidha kwenda kwenye miti, mifereji mikubwa au yapotelee tu katika mabonde, simaanishi mimi najua sana ila naomba tupeana mawazo kuwa haya maji yavunwe kitaalamu.













Kuna sehemu maji ni ya shida sana wangeweza kutumia maji haya yakiwa yametengenezwa kitaalamu Leo nawaachia homework hii tujadili kwa ufanisi.

Imeandaliwa na Buberwa Robert Blog
 

Thursday, 16 January 2014

ELIMU YA BURE KWA WAKULIMA NA WASIO WAKULIMA CHUKUA HII: JINSI YA KUPANDA, UMWAGILIAJI, UVUNAJI NA FAIDA YA MATUNDA AINA YA PARACHICHI . SEHEMU YA KWANZA

Sehemu ya Kwanza.. 
Kama ada kama dawa blog yetu inajieleza kwamba itakuwa inakumbusha au kutoa elimu ya vitu tunavyovijua lakini tumesahau au hatufuatilii, nah ii yote ni kutaka kukupa changamoto wewe msomaji ili uweze kufikiri njia nyingine ya kuweza kujiongezea kipato kupitia kilimo pia. 

Upandikizaji hujumuisha aina mbili za mimea. Unachukua mmea mmoja ambao unadhani hauna tija nzuri, na sehemu ya mmea mwingine ambao una ubora zaidi na kupandikiza kwa kukata na kufunga pamoja ili kupata mbegu bora zaidi.
 
Kwenye shamba la bwana Buberwa Robert, atakuwa na kitalu chenye zaidi ya miche 1500 ya miparachichi, ikiwa inasubiri kufikia wakati wa kupandikiza. 

Mbinu anayotumia
 
Kukusanya kokwa za parachichi kutoka maeneo ya sokoni; atakachofanya ni kuhakikisha tu kuwa mbegu hiyo ni safi, haijaathiriwa na magonjwa na itaota. Baada ya hapo huchagua zile zenye muundo mzuri na kuzipanda kwenye boksi au kwenye sehemu ya kitalu. Baada ya kuota ataziotesha kwenye makopo, au kwenye viriba kisha kuendelea kumwagilia maji mpaka zinapokuwa na umbo usawa wa penseli. Upandikizaji ni lazima ufanyike wakati mmea umefikisha unene wa penseli. Kupandikiza kwa kutumia chipukizi lililolingana na mche unaopandikizia ni njia yenye mafanikio zaidi.
 
Upandikizaji ni lazima ufanyike wakati ambao mizizi bado ni laini. Pandikizi litakalotumika wakati wa kupandikiza ni lazima lisiwe katika hatua ya ukuaji kwa wakati huo, na ni lazima umbo liwiane na mti linapopandikizwa kuzuia maji yasipotee na kusababisha pandikizi kukauka.

Mapandikizi ni lazima yatokane na aina ya parachichi ambazo zimeboreshwa kama vile HASS, FUERTE  au PUEBLA . Kwa wale wakulima ambao mmea utatoa majani mapya. wana mkataba na Africado, watahitaji kupata mapandikizi kutoka kwenye miti ya HASS. Hii ina maanisha kuwa mkulima anayetaka kuanzisha kitalu kwa ajili ya kupandikiza ni lazima apande walau miti 5 ya parachichi aina ya HASS ili kupata mapandikizi.
 
Njia ya kupandikiza ina ufanisi zaidi na ni rahisi kuliko kupanda miche upya, kwa kupandikiza inagharimu chini ya asilimia 75, kuliko kupanda miche upya na kuweza kupata aina ambayo inastahimili magonjwa. Wakulima pia wamekuwa na rekodi nzuri ya ongezeko la mavuno kutokana na mimea waliyopandikiza, pamoja na upungufu wa matumizi ya madawa.


Wakulima ambao wanafanya kazi zao chini ya CARITAS Njombe sasa wanaona faida kubwa inayotokana na kupandikiza, wameamua kuwekeza kwenye utaalamu huu na kuwa na miche mingi kwenye vitalu vyao. Hii ni mbinu ya kilimo ambayo ina faida kubwa kwa mkulima, huku akiwa amewekeza kwa kiasi kidogo sana katika kukabiliana na wadudu na magonjwa na kuepuka kuwa na mazao yenye ubora wa chini.

Usikose sehemu ya Pili ambapo Tutagusia zaidi katika suala zima la Namna ya Kupanda Parachichi, Faida na utapataje Kipato katika tunda hili usikose 


Wednesday, 15 January 2014

SIRI HII HAPA: HAYA NDIYO MAFANIKIO AMBAYO HUYAFAHAMU NA UNAYAPATA KATIKA BIASHARA YAKO.


Wote tunapenda biashara zenye mafanikio, lakini hatujui tufanye nini. Wengi tunaanzisha biashara ya kuiga tu, ingawa sijasema kuiga ni dhambi,basi utakuta salon hapa, pale, kule, nyuma, mbele pembeni yam taro wengine hata mteja akija anashukuru Mungu ndio anaagiza na chips kabisa ili afukie mashimo ya njaa.  Mbaya zaidi huduma kwa wate sio nzuri kwa kuwa biashara yenyewe haina lengo lolote zaidi mtu anajua kusuka, hakuna maandishi (Business Plan), lengo la biashara kuwa baada ya muda Fulani nikuze biashara yangu kwa kuongeza jingo labda nk.
 
Wengi tuna nunua magari ili yawe Taxi lakini hii Taxi haina mafanikio hata kidogo kwa kuwa dereva analalamika gari limekuwa si gari na sasa ni jinni, maana linbugia mafuta balaa, ukija kwa madereva wenyewe sasa hawana mission wala vision, wao ni kubambika tu bei mteja anapanda taxi mwaka mzima wewe umeng’ang’ania bei kubwa hadi anakukimbia, lakini kama ukijipanga kwa lugha, bei nzuri, service ya gari, uaminifu utafanikiwa.
 
Wakati najiingiza katika biashara nilikuwa nafanya kwa moyo mmoja kwa kutaka kushirikiana na wenzangu hata ikiwezekana tuchange tuweze kufanya biashara moja ambayo itazalisha na kupata faida kubwa.  

Lakini kumbe wenzangu walikuwa na malengo yao, walifanikiwa kuchukua mitaji kutoka kwangu na nilibaki masikini mwisho niliamua kuhamia katika biashara nyingine ambayo nilihisi itanizalishia.  Nilijiunga lakini bahati mbaya nilisahau kuwa hiyo biashara nipo na wale wale walioniangusha, na nilianguka kweli kwa kuwa nilipoteza fedha, nilipoteza marafiki,
niligombana na mke wangu, nilikuwa na madeni ambayo hadi leo ninaendelea kulipa.
 
Siri kubwa ya kufanikiwa ni kujifunza elimu ya namna ya kutafuta na kuendesha aina ya ile biashara unayotaka kuifanya, lakini pia ni vyema kubuni mradi unaoweza kuendelea, sio ule ambao unaanzisha leo, kesho unakufa.

Jambo linguine la msingi ni kujenga tabia  ya kuweka akiba.
Lakini la tatu kali zaidi ambalo wengi wetu huwa ni gumu ni ushirikiano wa watu zaidi ya wawili, ambao mna nia moja katika jambo moja mfano salon.
 
Ikiwa salon inahitaji vifaa vya kisasa basi hakikisha wazo lenu liwe la vifaa vya kisasa, mfano hesabu zenu ziangukie kuwa na viti 100 vya wateja wanaofanyiwa usafi wa nywele, viti 100 ambavyo kuna wateja, wanafanyiwa steaming, viti 100, ambavyo kutakuwa na wateja wanaoshwa miguu, viti 100 vya make ups, madawa yaliyoidhinishwa na TBS na TFDA ambayo hayadhuru mteja, huu ni mfano tu na pia unawea kuona katika picha nilizoweka.

Mnapokuwa mmeungana nguvu inakuwa ni kubwa kazi yenu ni kusimamia kila mmoja kujua anafanya kazi kwa umakini, analipwa kama mkataba unavyosema, usafi wa ofisi, lugha nzuri kwa wateja, ratiba zinaenda kama zilivyopangwa, wahudumu wanakuwa na muda wa kupumzika na huku wakiwa huru

kwa wenye ofisi katika kusema yao yaliyo moyoni, mfano kutoa mawazo yao na yakanyiwa kazi, mikutano ya kila wiki mfano jumatatu na ijumaa huwa inazalisha utendaji kazi uliomakini, lakini mikutano ya kila siku asubuhi au jioni kwa wenye biashara ni muhimu.
 
Mnaweza kujiunga watu 10 mabao mtaamua kuchanga labda 5,000,000/= kila mmoja ukipiga hesabu 5,000,000 x 10 = 50,000,000/= mnaweza kupanga kimkataba kuwa tutafanya kazi kwa umoja kwa miaka mitano baada ya hapo tutaangalia kama inalipa ili tuendelee, au kila mmoja aende kivyake.
 
Ili upate mafanikio kwa karne hii ya 21, ni lazima uweke ushirikiano na wenzako bila hivyo utaimba kama nguchiro, na kila siku utabaki kukataa na kuona kila jambo ni baya katika biashara yako.
 
Kitu kingine kikubwa ni kuwa na muda au ratiba maalumu na inayotekelezeka katika biashara yako, mteja akija anataka baridi katika chumba iwe baridi sio kila siku wewe unakuwa mama samahani au baba samahani, hawa Tanesco hawa, hapana ingia mkataba na kampuni la umeme wa jua, au upepo, ili

wateja wako wapate huduma ile ile au zaidi ya ile na sio kila siku unapunguza ukarimu kisa anakuja kwako hana pa kwenda, weka vitu kama vinywaji hasa hasa sharubati za kutengeneza mwenyewe kwa matunda ya msimu na yale yanayopatikana iwe katika hali ya usafi.  Au chukua paketi moja ya Tanga Fresh mtindi na ndizi tano mbivu sana weka katika blender hakikisha una blend kwa sekunde 40 hadi 60, wape bilauri ndogo wateja wako wawili wanywe utaona kesho watakuja kuuliza kama ulinunua wapi kinywaji kile, maana utakuwa umewasaidia sana kiafya, na ladha pia.  Hili ni somo nitakupa baadaye.
 
Biashara sio kila dakika ufikirie kupiga hesabu watakuja wangapi wateja, biashara ni jinsi gani kwanza hawa ulionao wataendeleaje kuja ili nao wakuletee wateja wengi, weka motisha au zawadi kwa wateja akikuletea wateja 10 yeye atapata shampoo moja au shilingi 10,000 au hata kufanyiwa huduma bure.
Mafanikio hutokana na jitihada katika maisha tunayoishi. Watu wengi wanaopenda kufanikiwa hutafuta mbinu mbalimbali za kutimiza ndoto zao. Je wewe unafanya nini kutimiza ndoto ambazo umekuwa nazo kwa miaka mingi kwamba nataka kuwa mfanyabiashara mkubwa. 
 Waza unipe jibu, tupeane mawazo.

Imeandaliwa na Buberwa Robert